Katika
kuhakikisha suala la elimu ya usalama barabarani inazingatiwa jeshi la polisi nchini kikosi cha usalama
barabarani kinatarajia kufanya maadhimisho ya wiki nenda kwa usalama barabarani
nchini, itakayofanyika mwezi October mosi huko mkoani Geita.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo, kamishuna msaidizi wa kikosi cha usalma
barabarani DCP Mohamed Mpinga amesema kuwa maadhimisho hayo yataenda sambamba
na kauli mbiu ya HATUTAKI AJAL, TUNATAKA KUISHI SALAMA, (No road crushes, we
want to live safely).
“Ongezeko la
vyombo vya moto nchini kwa upande mmoja na ule wa ongezeko la watumiaji wa
barabara wa ngazi mbalimbali hauna budi kutiliwa maanani, ili kuweza kuzuia
ajali za barabarani” Alisema kamishina Mpinga.
Pia alisema,
ajali nyingi barabarani zimekuwa zikichangiwa na wadau mbalimbali wa usalama
barabarani kutojua sheria pamoja nakutumia vyombo vya moto ambavyo ni vibovu,
hivyo kuathiri hali ya usalama barabarani.
Pia kauli mbiu ya
mwaka huu inasisitiza kila mtuaji wa barabara kufaham wajibu wake katika
kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa, na anasisitiza kuwa suala la
usalama barabarani siyo kazi ya kundi moja tu, bali ni la kila mtu anapaswa
kujiona ni muhusika.
“Wanahabari ni
miongoni mwa wahusika wa suala la usalama barabarani kwani kupitia wao wana
nafasi kubwa kuielemisha jamii na umma kwa ujumla ili kusaidia jitihada
mbalimbali katika kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria za uslama barabarani
nchini”
Kamishina Mpinga
aliongeza kuwa, wakati wa zoezi hilo jeshi la polisi kupitia kitengo cha uslama
barabarani litatoa elimu kwa wadau mbalimbali wa barabara pamoja na kufanya
ukaguzi wa vyombo vya moto ikiwemo magari, bajaj na pikipiki. Vilevile zoezi
hili litaendana na utoaji wa stika za usalama barabarani kwa vyombo
vitakavyothibitika kuwa na ubora wa kutembea barabarani.
Ambapo alivitaja
viwango vya ukaguzi wa magari na kuwekea stika itakuwa katika mifumo mitatu;
magari ya biashara yatatozwa shs 5000/-, wakati magari madogo ya binafsi shs
3000/-, pikipiki na bajaj shs 1000/-
Hivyo anawataka
wananchi kupeleka vyombo vyao vya moto katika vituo vya polisi kikosi cha usalama
barabarani kitengo cha ukaguzi wa magari ili kuweza kukaguliwa na kuhakikiwa.
“Endapo katika
ukaguzi wa chombo chochote kitabainika kuwa ni kibovu, basi mmiliki anapaswa
kukipeleka kwa ajili ya matengenezo, na kisha kukaguliwa kwa mara ya pili na
kubandikwa stika maalum”
Wakati huo huo
kampuni ya mafuta ya Puma Enegy ambayo imekuwa ikiwekeza kwa muda mrefu upande
wa barabara, ambacho inaamini ni kipengere muhimu katika maendeleo ya Taifa,
vilevile usalama barabarani umeendelea kuwa changamaoto kubwa duniani hivi sasa.
Philippe
Corsaletti ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Puma Enegy nchini amesema “tukumbuke kwamba
kuwekeza katika usalama ni kujenga nguvu ya baaadaye katika nyanja zote za
uwekezaji imara na kujenga uchumi endelevu kwa watu wetu”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni