Alhamisi, 23 Juni 2016

TBA YATEKELEZA AGIZO LA MAGUFULI LA KUDUMISHA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM.



Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha Agizo la Rais wa awamu tano wa Jamuhuri ya Muungano  Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  la kuyaweka mazingira katika hali ya usafi wafanyakazi wa  Wakala wa Majengo nchini (TBA)wamefanya usafi katika nyumba zinazo kaliwa na wafanyakazi hao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema  leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Elius Mwakalinga amesema kuwa hatua yawafanyakazi hao kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka nyumba zinazokaliwa na wafanyakazi hao kunafuatia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika mashirika na taasisi zinazomilikiwa na serikali .

‘’Sisi kama Wakala wa  Majengo ya serikali tumeamua kutekeleza agizo la Mheshimiwa Dkt.Magufuli la kudumisha usafi katika maeneo yetu ambapo hii leo tupo hapa Mikocheni Mtaa wa Alhaj Muhaj ambapo nyumba hizi zimekuwa zikimilikiwa na Mawaziri na viongozi mbalimbali wa serikali,” alisema Mwakalinga.

Katika hatua nyingine Mwakalinga alisema taasisi hiyo inaendelea kuwafuatilia wateja wake ambao hawajalipa kodi za majengo ambapo katika Mkoa wa Mwanza jumla ya wadaiwa sugu wa majengo 27 wanadaiwa na TBA.

Alisema kuwa taasisi hiyo inawadai wateja wake takribani shilingi bilioni 16 katika vipindi tofauti.Hata hivyo hatuja pata takwimu sahihi kwa wadaiwa sugu waliopo jijini Dar es Salaam.


Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari TBA , Edina Joseph amesema kuwa zoezi hilo lakuwafuatilia wadau sugu linaendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani .

Alisema kuwa hatua ya taasisi hiyo kufanya usafi katika maeneo ya nayozunguka katika nyumba zinazomilikiwa nataasisi  hiyo .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni