Alhamisi, 16 Juni 2016

SOKO LA HISA DSE LAFIKISHA SHILINGI BILIONI 35.7 NAKUWEZA KUVUKA LENGO.

i Afisa Mtendaji wa soko DSEMoremi Marwa





Timothy Marko.



HATIMAYE Soko la hisa la Dar es salaam DSE,limeweza kufikia malengo yake Baada ya kuuza hisa zake katika makapuni mbalimbali nakuweza kufisha shilingi Biloni 35.7 baada kuuza hisa 150000 kwashilingi 500 ambapo kampuni hiyo awali likuwa inahitaji shilingi bilioni 7.5sawa naongezeko 376 ya kiwango kilichokuwa kinahitajika na na soko hilo la mitaji nchini .

 



Akizunguza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji wa soko hilo Moremi Marwa amesema kuwa ongezeko hilo limechangiwa na wawekezaji wanje kuukuza mtaji wao kupitia soko hilo kwakiasi cha shilingi bilioni 25 wakati huo huo wawekezaji wa ndani waliweza kukuza mtaji yao kupitia soko hilo kwa shilingi bilioni10 .

 



‘’Kutokana namatokeo haya tumeweza kupata shilingi bilioni 22ambazo hapo awali hatukuwa tunazihitaji hapo awali hivyo basi kutokana namatokeo haya tunawahaidi wateja wetu nawawekezaji kupitia soko letu lahisa tutashirikiana na ili kiwango cha uwekezaji katika soko letu kiwezekuongezeka mara dufu ‘’’Alisema  Moremi Marwa .

 



Afisa Mtendaji wa Soko la hisa la Dar es salam Marwa alisema kuwa huu niwakati muhimu kwa wawekezaji kuweza kuwekeza mitaji yao kwa kununua hisa zinazotolewa na makapuni mbalimbali kupitia soko hilo .

 



Mkuu wakitengo cha ushauri wa kibiashara Kampuni Orbit Securites Co.ltd Laurean  Malawi wa soko lahisa la Dar es salaam linalo fursa nyingi katika kukuza mtaji nakuweza kujenga uchumi kwa wawekezaji wanaonunua hisa kupitia soko hilo .

 


Alisema kuwa kumeweza kuwa na maombi ya watu wengi ambapo jumla ya watu 3200 wanaomba kuwekeza katikasoko hilo kupitia masoko yamitaji nihatua kubwa hali hii hiyo inatoa dira kuwa soko hilo limeanza kukuza ushindani katika Masoko mengine ya mitaji barani afrika ikiwemo soko lahisa la Nairobi nalile lakutoJohanseburg  afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni