Jumatano, 15 Juni 2016

MFUMO WATAARIFA YA USAFIRI KUZINDULIWA KESHO.



Timothy Marko.
KATIKA Kuhakikisha dhana ya Mandeleo ya sayansi inakuwa hapa nchini nakuleta maendeleo hapa nchini Taasisi inayojihusisha nateknolojia yamawasiliano kurahisisha usafiri duniani  (UBA)imezindua mfumo wa upatikanaji wa taarifa za usafiri kwanjia yasimu hapa  nchini .

Akizungumza na waandishi wahabari kuhusiana namfumo huo wausafiri kwanjia yamtandao wasimu ambao utatarajiwa kuzinduliwa kesho katika hoteli ya Serena jijini Dar es salam  Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi hiyo hapanchini ambayopia makao makuu yake yapo nchini Marekani Alfred Msemo amesema kuwa mfumo huo utammuwezesha mtumiaji wa sekta yausafiri kujua taarifa mbalimbali za usafiri kwakutumia njia yamtandao wa Tehama uliopo kwenye simu .

‘’Mfumo huu una tripu sita ambazo mteja ataweza kutambua taarifa za usafiri na vyombo vyausafiri nchini ambapo mfumo huu  utakuwa unatumia mfumo wa tehama katika simu iliweza kupata taarifa mbalimbali za usafiri nchini .’’Alisema Afred Msemo .

Afred Msemo alisema kuwa mfumo huu tayari umeshaunganishwa katika miji mbalimbali duniani ambapo jumla ya miji sabini duniani tayari imeshaunganishwa namfumo huo isipokuwa Tanzania 
.
Alisema kuwa kutokana umaarufu wajiji la Dar es salaam duniani taasisi hiyo   imeona umuhimu kubwa wajiji hilo maarufu kuweza kuunganishwa na mfumo huo .

‘’Dar es salaam nimji wa 474 kuunganishwa na mfumo wa usafirishaji wa uba kwanjia yasimu duniani ilikuweza kupambana na changamoto za usafiri katika jiji la Dar es salaam’’Aliongeza msemo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni