Timothy
Marko.
SERIKALI
imelitolea ufafanunuzi juu ya madai ya kufukuzwa kwa wagonjwa wa seli nundu
kuweza kupata tiba katika hospitali ya taifa ya Muhimibili nakusisitiza kuwa
wizara ya afya haija sitisha huduma za wagonjwa wa seli nundu.
Akizungumza
Katika kongamano lililo wakutanisha wahanga wa ugonjwa wa seli mundu mapema hii
leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha magonjwa yasiyo yakuambukiza
katika wizara yaafya,jinsia na watoto nchini profesa Ayubu Magimba amesema kuwa
kusitishwa kwa huduma ya matibabu yaugonjwa seli mundu .
kwa muda katika Hospitali hiyo kumetokana
kuwepo kwa mradi ambao ulikuwa ukiwahudumia wagonjwa wa seli mundu kumalizika
muda wake nakusitiza kuwa huduma hiyo ya matibabu ya ugonjwa huo bado ipo
palepale .
‘’Nataka
kulitolea ufafanuzi suala hili wagonjwa wa seli nundu hawaja fukukuzwa Katika
hospitali ya muhimbili ila kulikuwa namradi wa kuwa hudumia watu wenye ugonjwa
wa seli mundu lakini hapo awali uliisha muda wake lakini hadi hivisasa huduma
za ugonjwa wa seli mundu zipo palepale ‘’Alisema Profesa Ayubu Magimba
Profesa
Magimba alisema kuwa serikali inawataka wagonjwa wa seli mundu kujiunga namfuko
wa bima ya afya ili kuweza kupunguza gharama za matibabu za ugonjwa huo .
Alisema
wizara hiyo inayokitengo maalumu chakutoa elimu cha ugonjwa huo ambacho kipo
kwenye kitengo cha magonjwa ya yasiyo ambukiza .
Takiwimu
zinaonesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya tano kwakuwa nawagonjwa wengi
katika ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara kuwa na wagonjwa wengi wa
selimundu ambapo zaidi watoto 300000 hufariki kutokana ugonjwa waseli nudu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni