Jumatano, 22 Juni 2016

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHA WASILISHA GHARAMA ZA UCHAGUZI NEC.



Timothy Marko.
HATIMAYE Chama cha Mapinduzi CCM kimewasilisha taarifa za Gharama za uchaguzi ulifanyika 25october mwaka jana ambapo taarifa hizo zikijumuisha Madiwani Ubunge Pamoja na Urais .

Akizungumza na waandishi wa habari katika makabidhiano ya taarifa za gharama za uchaguzi Mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkaguzi wa ndani wa chama hicho Stanslaus Mamilo amesema kuwa hatua hiyo inafuatia utekelezaji wa masuala ya kisheria ya sheria yauchaguzi inayowataka vyama vya vya siasa kuwasilisha gharama za uchaguzi mara baada ya uchaguzi kumalizika .

‘’Sisi kama chama chamapinduzi tunazingatia matakwa ya kisheria ikiwemo Gharama za uchaguzi ambapo taarifa hizi za gharama za uchaguzi hukokotolewa na Mkuu wa mahesabu ndani ya  chama nakuwasilisha katika tume ya uchaguzi ‘’Alisema Mkaguzi wa Mahesabu Stanslaus Mamilo .

Mamilo alisema kuwa Makabrasha hayo hupokewa na kitengo cha masijala yatumehiyo ikiwa niutekelezwaji wa gharama hizo zauchaguzi .

Katika hatua nyingine Mkuu wa masijala wa Tume ya Uchaguzi (NEC)Glacia Simbachawe  amesema kuwa hadi kufikia mchana wa leo nitakrbani vyama viwili tu ndio vilivyo wasilisha gharama za uchaguzi ambapo chama cha mapinduzi kinaongoza kikifuatiwa na chama ACT Wazelendo
 .
Msemaji wa Tume ya uchaguzi nchini Monica Laurenti alivitaka vyama vyasiasa nchini kuwezakuwasilisha gharama za uchaguzi katika tumehiyo 
.
Alisema kuwa vyama ambavyo vitaonekana vimevuka gharama za uchaguzi zitapelekwa kwa Mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali nakuweza kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu ili hatua za kinidhamu zichukuliwe .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni