Alhamisi, 26 Mei 2016

OFISI YA TAKWIMU KUSHIRIKIANA NABENKI YADUNIA KATIKA UKUSANYAJI WA TAKWIMU NCHINI.

Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha takwimu zinazotolewanchini zinakuwa na ubora wakimataifa nakuweza kutumika katika nyanja mbalimbali zakukuza uchumi Ofisi yatakwimu nchini kwakushirikiana na Benki ya dunia imeanzisha mpango endelevu wa maendeleo wa mwaka 2030.

Akizungumza na waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu waofisi yatakwimu nchini Dk.Albina Chuwa amesema kuwa mpango huo unalenga kuratibu viashiria 230 ambavyo vimeridhiwa na wakuu wa  takwimu duniani katikamkutano wake wa 47ulifanyika Newyork Marekani ambapo mpango huo ulalenga kuzisaidia nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania .

''MPANGO huu unakauli mbiu ya'' Leave no one BEHIND ''unalenga kuzisaidia nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ambapo mpango huu unalenga kuzalisha takwimu bora iliziweze kutumika katika nyanja za maendeleo ''Alisema Dk.Albina CHUWA .

Mkurugenzi chuwa amesema kuwa tasinia ya takwimu  inahitaji watu walionaweledi wakutosha wakuzikusanya,kuzichambua nakuweza kutafusiri matokeo ya sera .
Alisema kuwa kwakuzingatia unyeti wa sekta yatakwimu nchini ofisi ya takwimu imetetengeza mifumo mbalimbali itakayo wezesha kupata takwimu zilizo bora katika ukanda wa afrika mashariki .
''LENGO  lauanzishwaji wa mfumo huu unalenga kupunguza gharama zakusanya takwimu nchini nakuweza kupatamfumo mzima wa kuratibu shughuli nzima uandikishwaji wawapigakura nauandikishwaji waraia 'Alisema ALBINA chuwa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni