Jumanne, 5 Aprili 2016

HRLC:UCHAGUZI WA MWAKA 2015 ULIGUBIKWA NA KASORO NYINGI .


 Tokeo la picha la kituo cha sheria

Timothy Marko.
KITUO cha Haki za Binadamu nchini(HLRC) kimezindua ripoti ya mwenendo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo ripoti hiyo imetoa kasoro za zoezi zima la uchaguzi kuwa Chama tawala cha CCM Kilitumia rasmali za serikali ikiwemo magari yaserikali katika kufanya kampeni jambo ambalo nikinyume nasheria za uchaguzi.
 Akizingumza katika uzinduzi waripoti hiyo wakili wa kituo cha sheria na haki za binadamu  Hamisi Mkindi amesema hali yauchaguzi wa mwaka 2015 uligubikwa na idadi ndongo ya wapiga kura baada ya kutangazwa kwa uchaguzi wa marudio katika majimbo ya masasi ludewa na handeni hali iliyo changia idadi ndogo ya wapiga kura.

''kumekuwa na tuhumaza udanganyifu wa matokeo ya uchaguzi tulienda katika majimbo yamasasi ,ludewa Handeni ,kwani uchaguzi wa marudio watu hawakujitokeza kwa wingi katika majimbo hayo niasilimia 3.9 tu yakura zilizkuwa zimeharibika ''Alisema wakili wakituo chasheria Hamisi MKINDI .

WAKILI  MKINDI alisema kuwa baadhi yavyama vyasiasa vilikuwa naruzuku ndogo kutoka serikalini vilishindwa kufanya kampeni hali ili yofanya kuwa nauwakilishi mdogo katika kampeni katika majimbo yote yauchaguzi ..

Alisema kuwa kasoro nyingine iliyojitokeza ni serikali  kuridhia sheria ya mtandao haraka haraka bila kuwashirikisha wadau mbalimbali wa uchaguzi.

''Kasoro nyingine niwaangalizi kutoruhurisiwa katika zoezi laujumlishwaji wamatokeo ikiwemo kupewa fursa yakuangalia zoezi hilo la ujumlishwaji ''Aliongeza WAKILI Mkindi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni