Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Ijumaa, 4 Machi 2016
NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ZA JITATHIMINI KATIKA UCHAGUZI ILI KUKUZA DEMOKRASIA
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha Demokrasia inakuwa katika nchi za afrika Mashariki, nchi hizo zimekutana nchini Tanzania kuweza kufanya tathimini juu yaukuaji wa demokrasia katika mchakato wa uchaguzi unaofanyika katika nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mbuge wa bunge la Afrika Mashariki nchini Tanzania Benard Mulunya amewataka nchi hizo kuweza kujitathimini jinsi serikali za afrika mashariki zinavyoendesha chaguzi zake .
''Katika Tathimini tuliozozifanya nchi za afrika mashariki zimekuwa nakasoro nyingi katika kuendesha demokrasia hususan Katika uchaguzi mkuu hivyo leo tumekutana kujadili changa moto katika chaguzi za afrika Mashariki''Alisema Benard Mulunya .
Mulunya alisema kuwa mwendo wa uchaguzi katika nchi za afrika mashariki zimekuwa zikigubikwa nakutokuwa tume huru,serikali iliyopo madarakani kuendesha uchaguzi nakusababisha demokrasia kutoweza kupatikana kwa misingi ya haki .
Alisema Nchi nyingi za Afrika mashariki zimekuwa zikabiliwa na ukosefu wa bajeti nakutegemea nchi wahisani kutoka nje kuweza kufadhili uchaguzi hali inayopelekea ufinyu wa demokrasia
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni