Jumanne, 29 Machi 2016

MABALOZI WA VYUO VIKUU WAPATA ''DILI '' SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM.



Tokeo la picha la patrick mususa

Meneja MAUZO na Biashara Patrick Mususa

Timothy Marko
SOKO la hisa la Dar es salaam limewateua mabalozi wa vyuo vikuu kufuatia shindano la scholar Investment challenge ili kuweza  kutangaza huduma zinazotolewa na soko hilo .

Akizungumza na waandishi wa Habari Mapema hii leo jijini Dar es salaam Meneja Mauzo na Biashara amesema kuwa mabalozi walioteuliwa nipamoja na chuo cha IRP ,chuo kikuu cha Dar es salaam ,sokoine ,IFM ,pamoja nachuo kikuu cha Dodoma

‘’Wanafunzi 500 wavyuo vikuu wameweza kushiriki katika shindano letu la Scholar Investment challenge ambpo wanafunzi hawa watakuwa mabalozi wetu katika vyuo mbalimbali ‘’Alisema Meneja Biashara na Mauzo Patrick Mususa  
Mususa alisema kuwa kupitia mabalozi hao wa vyuo vikuu nchini wataweza kukuza hamasa kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali kuweza kushiriki katika shindano hilo .
Alisema kuwa kila chuo kitakuwa namabalozi watano ambao watahamasisha wanafunzi kujiunga nashindano hilo ambalo linaendelea .
‘’Ninatoa wito wanafunzi wavyuo vikuu nchini kuweza kujitokeza katika shindano hili ilikuweza kuwa mabalozi wetu wa soko lahisa ili kuweza kupata fursa mbalimbali za kujijenga kiuchumi ‘’Aliongeza Mususa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni