Timothy
Marko.
WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amezindua
programu itakayowezesha uimarishaji wa utendaji wa mawasiliano katika taasisi
itakayo wezesha utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini
.
Akizindua Programu hiyo mapema hii leo jijini ,Waziri Lukuvi
amesema kuwa uzinduzi wa program hiyo utawezesha uwazi wa mikataba yauwekezaji
kwenye mashamba makubwa kwa kuwa nautaratibu wa ugawanaji faida zinzotokana na
uwekezaji katika ardhi.
‘’ Progamu hii itawezesha taasisi mbalimbali kuwa na uelewa wa
sera ,sheria na taaratibu za ardhi pamoja na uimarishaji wa njia za
mawasililiano kati ya tasisi ilikuweza kutatua migogoro ‘’Alisema Waziri
William Lukuvi .
Waziri Lukuvi alisema kuwa pragamu hiyo itawezesha hatua
mbalimbali ikiwemo za kurasimisha miliki za kimila katika wilaya .
Alisema kuwa katika hatua za awali za utekelezaji wa progamu hiyo
utahusisha uboreshaji wa sera ,sheria katika taasisi kwenye sekta nzima ya
ardhi na utekelezaji wake utatambulika kitaifa .
‘’Mpango huu utajumuisha wilaya za ulanga na kilombero mkoani
Morogoro katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kuanzia ngazi ya
wilaya hadi vijiji upimaji wa vipande vya ardhi pamoja na utoaji wa hati za
haki miliki yakimila ‘’Aliongeza Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam
LUKUVI .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni