Timothy Marko.
SAKATA la uchaguzi wa Mamea wa mkoa wa Dar es salaam uliofanyika Jumamosi iliyopita Katika ukumbi wa Karimjee umechukua sura mpya baada ya jeshi lapolisi kanda maalum katika mkoa wa Dar es salaam kumuweka Rumande hii leo kwa muda usijulikana Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwakosa la kutoa maneno ya Kashfa kwa aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo wa mamea (RAS).
Tukio lakumtia Hatiani Mbuge huyo wa Kawe Halima Mdee linafuatia Baada ya Mahojiano Maalum ya liyofanywa na mkuu wa upelelezi wa kanda hiyo kwamuda wamasaa sita,Sambamba nakushikiliwa na jeshi hilo lapolisi pia Jeshi hilo linawashikilia Madiwani wa Chama cha Demokasia na Maendeleo Humprey Sambo ambaye nidiwani wa kata ya Mbezi,Shafi Juma diwani wakata ya saranga kwakuhusika navurugu katika uchaguzi huo.
Awali katika mahojiano maalumu nawaandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Profesa ABDALAH SAFARI aliwaambia waandishi wa habari kuwa Halima Mdee anatuhumiwa kwakosa lakumshambulia Ras kwa kosa mbalo Hana hatia nalo .
Profesa Safari alisemakuwa Mara nyingi wanachama wachama hicho wamekuwa wakituumiwa na jeshi hilo pindi chama hicho kinapofanya uchaguzi nakuweza kuwashikilia viongozi wake nakuwa weka hatiani.
''SISI tunasema hawa polisi wanatumika kisiasa kwani Halima Mdee alikuwa anatakiwa kupewa Dhamana kwani nihaki yake lakini amenyimwa haki hiyo nilazima jeshi hili libadilike nakutotumiwa kisiasa ''Alisema Profesa Safari.
Chanzo chetu ambacho hakikutaka kutajwa jina Kili dai kuwa Mbuge Wa Kawe Halima Mdee alishikiliwa na polisi baada ya askari sita waliovaa kuzunguka katika nyumba yake iliyopo kawe jijini Dar es salaam na mbuge huyo kutoka katika nyumba yake nakuanza kurumbana na polisi walio vaa kiraia ndipo askari hao kurudi kituo cha Central kilichopo Posta kuchukua kibali cha kumkamata mbunge huyo .
chanzo kilisema kuwa baada yamvutano napolisi ndipo Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Dar es salaam kutoa kibali cha kumkamata kiongozi huyo kwa mahojiano maalum.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni