Alhamisi, 31 Desemba 2015

TANZANIA YASHIKA NAFASI 82 KWA MAZINGIRA YA KIUCHUMI DUNIANI .



Timothy Marko.
TANZANIA imekuwa nchi ya 82 kati yanchi 100 duniani zenye mazingira huru yakiuchumi  kwakipindi cha mwaka huu ikilinganishwa nafasi92 mwaka jana kwamujibu wa ripoti ya uhuru wa  uchumi wa Dunia(Economic Freedom of the world Repot) .

Ripoti hiyo imetolewa na Mkurugezi mtendaji wa taasisi ya Uhuru Intiative Policy Education Isack Danford ambapo amesema kuwa vigezo vilivyoweza kuiwezesha nchi ya Tanzania Kushika nafasi hiyo nikutokana na kuwepo kwa mifumo ya udhibiti wa bishara za ndani ,kudhibiti vitendo vya hongo,upendeleo wa utoaji huduma kwa umma na gharama za huduma katika ofisi za umma zinazotokana na urasimu.

‘’Masuala mengine yaliyoweza kuifikisha Tanzania katika nafasi ya 82 nipamoja na kuwepo kwa mahitaji yakiutawala ,ulazimishaji wa kuchangia huduma za kiserikali pamoja na makubaliano ya Mishahara ‘’Alisema Isack Danford .

Mkurugenzi Danford alisema kuwa viwango vingine vilivyopelekea  Tanzania kushika nafasi hiyo nipamoja na kuwepo kwa vikwazo katika uwekezaji ambavyo visivyo vya kiforodha nakuwepo kwa utofauti wautowaji waviwango vya forodha .

Alisema kuwa sambamba naviwango hivyo kupungua kwa thamani shilingi ya Tanzania katika soko ladunia imechangia Tanzania kushika nafasihiyo ya 82 ikilinganishwa na nchi za afrika mashariki .
‘’Nchi nyingine zilizo kuwa katika ukanda wa afrika mashariki nipamoja na Kenya ikishika nafasi ya sitini ambayo ilikuwa nikinara katika uchumi katika ukanda wa afrika mashariki  ,wakati Ruwanda ambayo sasa inashika nafasi yakwanza katika afrika mashariki inashika nafasi thelathini na nne na Uganda inashika nafasi yamwisho katika nchi za ukanda wa afrika mashariki ikishika nafasi ya arobani duniani ‘’Aliongeza Isack Danford .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni