Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Alhamisi, 10 Desemba 2015
SAMIA: Serikali tutaendelea kuboersha mazingira ya Upatikanaaji wa haki Nchini.
Timothy Marko.
KATIKA kuadhimisha siku ya Haki za binadamu nchini Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha mazingira ya upatikanaji wa haki nchiniikiwemo kuzisimamia taasisi za utoaji haki ilikuhakikisha taasisi hizo zina simamia majukumu yake na kutekeleza wajibu wake ipasavyo
.
Akizungumza Katika kilele cha maadhimisho cha siku ya haki za binadamu yanayofanyika Desemba 10 kila mwaka jijini Dar es salaam Makamu wa RAIS wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya matukio ukikwaji wa hakiza binadamu ambapo matukio hayo nipamoja namauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualibino ,mauaji ya wanawake vikongwe ,mahabusu kukaa muda mrefugerezani bila kusikilizwa .
‘’Serikali ya awamu ya tano imejipanga kutomeza vitendo vyote vya ukiukwaji wa haki za binadamu bila kumunea haya mtu ,sambamba na hili serikali hii itahakikisha kuwa mchakato wa katiba mpya unazingatia haki za binadamu endapo itapitishwa ‘’Alisema Makamu wa Rais SAMIA SULUHU .
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU alisema kuwa serikali ya awamu yatano imedhamiria kuhakikisha Haki za wananchi zinatekelezwa ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na ufisadi .
Alisema kuwa serikali itaivalia njuga masula mazima ya ufisadi pamoja na ubadilifu na ufujaji wa mali za umma kwa kuweza kusimamia sheria nakuhakikisha watuhumiwa waote wa ufisadi wana fikishwa katika vyombo vya sheria .
‘’Mathalani watuhumiwa wote watafikishwa katika vyombo vyasheria bila kumonea mtu yeyote ikumbukwe kuwa ubadhirifu wizi katikaumechangia kudumaza uchumi ‘’Aliongeza Makamu wa RAIS SAMIA.
Mwenyekiti wa Tume ya HAKI za binadamu Bahame Nyanduga amesema kuwa ingawa hali ya haki za binadamu hapa nchini inaendelea kuimarika lakini taasisi hiyo ya umma inakabiliwa na changamoto ikiwemo mauaji yawatu wenye ulemavu wangozi ,wanawake wazee ,ukatili kwa watoto
.
Alisema kuwa wajibu wakulinda haki za binadamu sio jukumu la taasisi hiyo bali nila kila mwananchi hivyo kila taasisi inawajibika katika kulinda haki za binadamu .
‘’Wajibu wakulinda na kuhifadhi haki za binadamu ni wetu sotekwa maana serikali asasi za kiraia sekta binafsi ,mtu mmoja moja najamii kwa ujumla ‘’Alisema Bahame Nyanduga.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni