Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumanne, 29 Desemba 2015
NGOMBE 79 WAUWAWA KUTOKANA MIGOGORO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA .
Timothy Marko .
JUMLA ya ng’ombe 79kwa kipindi kinacho ishia mwezi Desemba mwaka huu wameweza kuuwawa kutokana na migogoro ya wafugaji inayoendelea wilayani MVOMERO Mkoani Arusha .
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkuu wakitengo cha Habari na mwasilano wizara ya Mifugo ,kilimo na uvuvi JUDITH Mhina amesema kuwa kumekuwa naukiukwaji wa haki za wanyama katika wilaya hiyo kutokana kuuwawa kwa wanyama hao pasipokuwa nakusudio maalum kwa wanyama hao .
‘’Hawa wanyama pia wana haki ya kuishi kama ilivyoku wa kwa binadamu ,tumekutana leo kutoa masikitiko yangu kutokana na vifo hivi vya wanyama na wa fugaji vinavyo tokana namigogoro ya wafugaji’’Alisema JUDITH Mhina .
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano JUDITH Mhina amesema kuwa kutokana nakuwepo kwa migogoro hiyo baina ya wakulima na wafugaji wizara yake imeamua kushirikisha wizara nyinginezo ikiwemo wizara ya ardhi ili kuweza kutenga nakuanisha matumizi bora ya ardhi ilikuweza kuepukana na migogoro hiyo.
Alisema kuwa Nivema wananchi waweze kutoa taarifa za matumizi mabaya ya ardhi kwa wakuu wa wilaya ,vitongoji namikoa ili waweze kuwachukuliwa hatua za kisheria .
‘’Wananchi wenyewe wanapoona kuwa kuna matumizi mabaya ardhi watoe taarifa hizo kwa serikali mapema kwa kushirikisha wakuu wa wilaya ,Halimashauri,mikoa na vijiji ili waweze kuchukuliwa hatua ‘’Aliongeza MHINA .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni