Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatano, 16 Desemba 2015
ACT WAZALENDO YATOA TAMKO JUU YA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI BURUNDI.
TAARIFA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KWA VYOMBO VYA HABARI
JUU YA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI BURUNDI
TANZANIA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI IKOMESHE MAUAJI NCHINI BURUNDI
CHAMA cha ACT-Wazalendo kinasikitishwa sana na maujai yanayoendelea nchini Burundi na hasa Mji Mkuu wa nchi hiyo Bujumbura. Hali hii ya mauaji imesababishwa kwa kiasi kikubwa na uamuzi wa Rais wa sasa wa nchi hiyo Ndugu Piere Nkurunzinza kuendelea kugombea na hatimaye kuchaguliwa kuwa Rais wanchi hiyo katika mazingira yanayodaiwa kuvunja demokrasia na utawala bora.
Tangu machafuko hayo ya nchini Burundi yaanze zaidi ya watu 100 wameshauawa kufikia wiki hii na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Aidha, wimbi la wakimbizi kutoka Burundi linarudi kwa kasi na wengi wao wakikimbilia nchini Tanzania.
Bahati mbaya sana mpaka sasa Jumuiya ya Kimataifa na hasa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Burundi ni mwanachama, haikuchukua hatua za maana za kuzuia kuchafuka kwa utawala wa kidemokrasia na utawala washeria nchini Burundi, na wala haichukui hatua stahiki kuzuia mauaji yanayoendelea
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni