Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Ijumaa, 27 Novemba 2015
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka waalimu nchini kujiunga na Taasisi za kifedha
Timothy Marko.
WAZIRI MKUU wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amewataka walimu nchini kujiunga katika Benki yawalimu(MCB BANK ) ilikuweza kupata fursa ya kuwekwa kwenye orodha katika soko la mitaji lilopo katika soko lahisa la Dar es salaam ilkuweza kukuza uchumi wao ilikuondokana na umasikini .
Akizungumza katika uzinduzi wa kuorodheshwa kwa Benki yawalimu nchini katika soko la hisa la jijini Dar es salaam DSE Waziri KASIMU Majaliwa amesema kuwa nivyema walimu nchini kujiunga na taasisi zakifedha ikiwemo benki hiyo ilikuweza kukua kiuchumi nakuepuka visingizio visvyokuwa na tija .
‘’Tuepuke kutoa visingizio vya aina mbalimbali ikiwemo suala la umbali kutokana na matawi ya benki hii ya walimu kuwa na matawi machache hata kama ukiwa Ngara ,Mtwara ,Arusha ,chunya,lakini Bado kuna unaweza kufungua akaunti yako katika tawi labenki yawalimu lilipo Dar es salaam kwa kutumia mawasiliano ya kisasa.’’Alisema Waziri mkuu Kasimu Majaliwa .
Waziri mkuu Majaliwa alisema kuwa Benki hiyo imekuwa namikakati madhubuti yakuwafikia watanzania wote kwa muda muafaka lakini kumekuwa nachangamoto mbalimbali zakukuza huduma yakifedha kwa wadau hao wa sekta elimu .
Alisema kuwa sekta ya teknolojia ndio njia sahihi yakuwakutanisha wadau hao muhimu katika Nyanja ya elimu katika kutumia taasisi za kifedha ikiwemo Benki hiyo ya walimu ilkuweza kujikwamua na umasikini na kukuza uchumi wao .
‘’ Tunayofursa benki yetu kuorodheshwa katika orodha katika soko la hisa hata hivyo tusibweteke tuendelee kufanya kazi kwa bidii nakutumia fursa hizi zilizopo mbele yetu ikiwemo benki ya walimu ili kuweza kuboresha maisha yetu ‘’aliongeza waziri MKUU KASIMU MAJALIWA .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni