Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 23 Novemba 2015
WAWEKEZAJI 2500 WAWEKEZA KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM
Timothy Marko.
JUMLA ya wawekezaji wa soko la mitaji wa patao 2500 wameweza kuwekeza katika soko la hisa la jijini Dar es salaam (DSE)ambapo idadi ya ongezeko hilo nikutokana wawekezaji hao kutumia njia ya mtandao wa simu katika kununua hisa zake .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salam Meneja Mauzo na biashara Patrick Msusa amesema kuwa ongezeko hilo la waekezaji ni asilimia 20.5 ikilinganishwa 20.8 kwakipindi cha wiki iliyopita .
‘’Wawekezaji wameongezeka hadi kufikia 2500 ikilinganishwa na kipindi cha awali hali hii imetokana wawekezaji kutumia njia yasimu katika kununua hisa za soko letu ‘’Alisema Meneja Biashara na Mauzo Patrick Msusa.
Patrick Msusa amesema kuwa hali hiyo imeweza kuchangiwa na sekta ya viwanda kukua ambapo jumla yamakampuni matatu yaliweza kuwekeza katikasoko hilo kwa kuuza hisa zake katika soko hilo la hisa .
Alisema kuwa Makampuni ya Dar es salaam Commercial Bank (DCB),benki ya CRDB pamoja na Tanzania BREWRIES limited ndiyo yanayoongoza kwa kuuza hisa zake kupitia soko hilo .
‘’idadi ya mauzo ya hisa yameongezeka kutoka shilingi bilioni2.7 hadi kufikia shilingi bilioni 4.2 kwakipindi cha wiki iliyopita ambapo nisawa na asilimia 57’’Aliongeza Meneja biashara MUsusa .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni