Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatano, 18 Novemba 2015
PSPF NA NHIF YAANZA UTEKELEZWAJI WA KAULIMBIU YA RAIS MAGUFULI KATIKA SEKTA YA AFYA.
Timothy Marko .
KATIKA kuhakikisha afya za wananchi zinaimarika nchini mfuko wa bima ya afya(NHIF) na mfuko wa pesheni wa PSPF wameanzisha mashirikiano ya pamoja ilikuwawezesha wananchi hao kuweza kupata huduma stahiki ya afya ikiwa ni moja ya utekelezaji wa sera ya chama cha mapinduzi(CCM) iliyotolewa na Rais wa jamuhuri yamuungano wa Tanzania Jonh Pombe Magufuli wakati akiomba ridhaa kwa wananchi kushika kiti cha urais ambapo alitoa ahadi yake kuwa atakapo ingia madarakani ata hakikisha watanzania wote wanapewa bima ya afya .
Akizungumza katika uzinduzi wa fao la matibabu kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari wa matibabumapema hii leo jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa bima ya afya NHIF Michael Muhando amesema kuwa taasisi hiyo ya serikali imelenga kuwa fikia makundi yote ya jamii yaliyo kuwemo kwenye sekta rasmi naile isiyo rasmi ili kuweza kuboresha afya za wananchi wote .
‘’Mfuko huu wa bima ya afya umelenga kuwafikia makundi yote ya sekta rasmi pamoja na sekta isiyo rasmi kwa gharama ya shilingi 76800 mpango huu tunashirikiana na sekta zote za kibenki ambapo jumla ya vikundi 37 vya wajasilimali tayari vimeshaingia kwenye mpango huu ‘’AlisemaMkurugenzi wa mfuko wa bima ya afya NHIF Michael Mhando.
Mkurugenzi Michael Muhando alisema kuwa kutokana na kauli mbiu ya Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Jonh Magufuli ‘’HAPA KAZI TU’’kaulimbiu hiyo inatekelezwa kikamilifu baada ya makampuni hayo ya umma kuimarisha nguvu katika kutatua changamoto za huduma za afya .
Alisema kuwa ushirikiano huo wa mfuko wa pesheni wa PSPF pamoja na bima ya afya NHIFutaweza kuwasaidia wastaafu wa sekta mbalimbali za umma na binafsi kuweza kuboresha afya zao .
‘’Ile slogan inayosema hapa kazi inatekelezwa kikamilifu kwa kuunganisha mifuko yote miwili ilkuweza kutatua changamoto ya huduma yamalipo ya afya na utoaji wa huduma hii bure kwa wananchi kama ilivyo aidiwa na mheshimiwa Rais ‘’Aliongeza Michel Muhando .
Katika hatua nyingine MKurugenzi Mkuu wa PSPF Adamu MALIMU alisema kuwa taasisi hiyo inaendeleza mpango mkakati wakuwasajili wanachama wake katika mpango wa hiari baada ya kufanyia utafiti wanapata huduma za afya kwa kutumia bima yaafya ni wachache na kuongeza idadi ya wanachama wa mfuko wa bima ya afya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni