Jumatano, 2 Septemba 2015

SERIKALI:TUNAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA ZA MASHEHE NCHINI KONGO

Timothy Marko.KUFUATIWA kuwepo taarifa za kukamatwa kwa baadhi ya Raia wa Tanzania huko nchini kongo ambao wadaiwa kuwa ni Viongozi wa dini ya kiisilam wakiwa wakitoa huduma yakidini katika nchi hiyo,Serikali ya Tanzania imesema kuwa imejaribu kufanya mawasiliano na nchi hiyo yakongo ili kuwa pata taarifa za viongozi hao nakuwa viongozi hao wakidini hiyo wako huru .
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje Liberata Mulamula amesema kuwa bado serikali inaendelea kufuatilia taarifa hizo kutoka nchini Kongo kwa ukaribu zaidi baada ya kumtuma balozi wa Tanzania nchini kongo kufuatilia viongozi hao wa dini yakisilam waliopo kivu ya kaskazini nchini humo kwani taarifa za awali zinaonesha haijawahi kuwekwa kwa raia Tanzania Kizuizini pindi wanapo wasili katika nchi hiyo.
''Kwa ujumla Watanzania hawajawahi kukamatwa mateka hii ni Mara ya kwanza kuzuiliwa kwa mashehe hawa wakiwa katika huduma yakidini nchini Kongo tuna endelea kuwasiliana na serikali yakongo ilikupata taarifa juu yamashehe hawa''Alisema Liberata Mulamula .
Mulamula alisemakuwa bado serikali inaendelea kuwasiliana na nchi hiyo kwani baada yakupata taarifahizo katika vyombo vya habari serikali ilishitushwa na nataarifa hizo za kukamatwa kwa mashehe hao .
Alisema kuwa nijambo lakawaida kwa raia kutoka Tanzania kuhubiri neno lamungu katika nchi hiyo .
''Nikawaida kwa raia watanzania kwenda kuhubiri nchini Kongo lakini Taarifa za awali zinaonesha viongozi hawa wakidini wameshikiliwa nakikundi cha waasi waliopo nchini kongo''Aliongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni