Ijumaa, 4 Septemba 2015

SERIKALI YAZINDUA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI .

Timoth Marko.Serikali
imezindua mfuko maalum wa fidia kwa wafanyakazi wa taasisi za umma utakao wawezesha watumishi hao wa umma kupata mafao mbalimbali ikiwemo kumia kazini ama kufariki kwa mtumishi wa umma wakati akiendelea kutumikia taifa lake .Akizungumza katika ufunguzi wa mfuko huo jijini Dar es salaam mapema hii leo Waziri wa kazi na ajira Gaudencia Kabaka amesema kuwa uanzishwaji wa mfuko huo unafuatia sheria ya fidia kwa wafanyakazi Na 20 ya mwaka 2008 baada ya marekebisho yasheria yamwaka 1949 baada kuwepo kwa changamoto katika utekelezaji wake.
''Mafao yalikuwa yakitolewa na mfuko huu yalikuwa ni machache katika sheria ya zamani ambapo kiwango cha fidia kilikuwa nikidogo sana nakutokidhi mahitaji ya sasa ya wafanyakazi pindi wanapo ugua ama kuumia ,nakufariki dunia kutkana na kazi wanazofanya ''Alisema Gaudencia Kabaka .
Gaudencia Kabaka alisema kuwa uanzishwaji washeria yakazi ya mwaka 2008 utawezesha kuboresha mafao kwa wafanyakazi na kuboresha viwango vya fidia kwa wategemezi na wafanyakazi .
Alisema kuwa mchakato wakufuatilia mafao hayo, kwa wafanyakazi hauto kuwa wakipindi kirefu bali utachukua muda mfupi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma .
''Kazi niliyopewa kwa siku hii ya leo nikuzindua bodi ya wadhamini wa mfuko wafidia kwa wafanyakazi ambapo bodi hii imeundwa kwa mujibu wa sheria kazi kifungu cha 12 pamoja nakifungu cha 20 cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi ya mwaka 2008 ikiwajumuhisha wajumbemalimbali wa serikalini ''Aliongeza Waziri wakazi najira Gaudencia kabaka .
Waziri Kabaka aliongeza kuwa wajumbe wabodi hiyo watajumuisha vya ma vya wafanyakazi ,vyama vya waajiri ,osha ,benki kuu Pamoja na taasisi za elimu ya juu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni