Timothy Marko.IMeelezwa kuwa jumla yawatu milioni tatu hufariki kutokana kukosa lishe bora kila mwaka ambapo zaidi ya watu hao wanatokea katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara ,wakati huo huo nchi ya Tanzania imekuwa ikishika nafasi ya tatu wakati nchi yaburundi ikishika nafasi yapili Huku nchi ya jamuhuri ya kidemokrsia ya watu wakongo(DRC)ikishika nafasi ya kwanza kwa vifo vitokanavyo naugonjwa wa ukosefu wa lishe bora .
Akizungumza nawaandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Michael Jonh amesema kuwa jumla yawatu milioni 161.1 hupata ulemavu wa viungo haliinayochangiwa na ukosekanaji wa lishe bora ambapo hali hiyo imechangiwa baadhi ya watu hususan watoto kuwa naupungufu wa madini ya zinc ambayo hupatiaka kwa kula chakula bora ambavyo vina virutubisho vyote mwilini .
''Hali ya lishe Duni huchangiwa na upungufu wamadini yazinc pamoja na madini joto mwilini hali hii ya upungufu wa madini haya katika mwili hupelekea magonjwa ya utapia mlo nahatimaye kupekea hata vifo kutokana nakutopata lishe bora ''Alisema Michael Jonh .
Jonh alisema kuwa kufutia Janga hilo la lishe duni Serikali kwakushirikiana nawadau mbalimbali wa sekta ya afya wameanzisha Kampeni maalum ikiwemo kutoa elimu kwa wafanyabishara wa vyakula ili waweze kuzingatia kanuni za uandaji wa vyakula vinavyo zingatia virutubishi muhimu mwilini ilikuondokana najanga hilo.
Alisema kuwa serikali inatarajia kuendesha washa maalum itakayo anza septemba 9 mwaka huu jijini Arusha ambapo kongamano hilo linalenga kutoa elimu ya virutubishi katika vyakula ili elimu hiyo iweze kuwa fikia watu wengi zaidi na kuondokana na tatizo hilo .
''Tunatarajia kuanzisha kongamano maalum la Lishe katika jiji la arusha ilikuweza kutoa elimu juu ya umuhimu walishe bora nakuongeza virutubishi muhimu katika vyakula ili kuondokana na tatizo hili ''Aliongeza Kaimu katibu Michael Jonh.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni