Jumanne, 5 Agosti 2014

CHUO KIKUU CHA KAMPALA CHA KANA MADAI YA KUKOSA UBORA .


Timothy Marko.
KUFUATIA kuwepo kwa tuhuma za kuwepo kwa vyuo vingi vinavyotoka nje ya ya Tanzania kutokuwa na ubora unaotakiwa kwa hapa nchini chuo kikuu cha kampala cha nchini Uganda tawi la Dar es salaam KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY (KIU)kimekanusha madai hayo na kueleza kuwa chuo hicho kimepata ithibati nakusajiliwa kutoka tume ya vyuo vikuu hapa nchini (TCU).

Akizungumza na waandishi wa wahabari jijini leo,Mkurugenzi wa masoko na mahusiano ya umma wa chuo hicho cha KIU  ,Thomas some amesema kuwa tuhuma zinazotollewa na baadhi ya watu kuhusiana na usajili wa chuo hicho si za kweli nakubainisha kuwa kumekuwa na baadhi ya wafanyakazi walio fukuzwa chuoni hapo wamekuwa wakichafua taswira ya chuo hicho .

‘’kumekuwa na baadhi ya wafanyakazi walifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu wamekuwa wakieneza tuhuma juu ya chuo chetu lakini tuhuma hizi siza kweli kwani chuo chetu kinatambuliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania commission university (TCU)’’alisema Thomas some  .
Thomas Some alieleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya wahitimu waliomaliza chuoni hapo nakuweza kuajiliwa katika hospitali ya taifa yamuhimbili kwa ngazi ya uangalizi wa madawa medical .

Some alisisitiza kuwa hivi karibuni Raisi mstaafu wa awamu ya pili ALLY Hassan Mwinyi alikubali kwa dhamira yake kuwa mshauri wambo ya kitaluma chuoni hapo nakusisitiza kuwa kama chuo hicho kisinge kuwa na ithibati Rais huyo wa awamu yapili hapa nchini asingeweza kukubali kuwa mshauri wa chuo hicho ili hali chuo hicho hakitambuliki na tume ya vyuo vikuu TCU hapa nchini.

‘’HIVI karibuni Rais wa wawamu yapili wa Tanzania ALLY HASSAN MWINYI ambaye ni Rais mstaafu alikuja chuoni kwetu na kukubali yeye mwenyewe kuwa Chancellor wa chuo chetu kama chuo chetu kinge kuwa hakitambuliki Rais mwinyi asingeweza kukubali kuja chuoni kwetu kuongea nasi kwachuo ambacho hakitambuliki.’’aliongeza Mkurugenzi wa masoko wa chuo hicho Thomas same.

KATIKA hatua nyingine chuo hicho kimeanzisha progamu mpya ya masomo ya Bursal Scheme ambayo inamuwezesha mwanafunzi aliyepo chuoni hapo kuweza kupata huduma za masomo kwa punguzo la asilimia hamsini hususan kwa wanafunzi wakitanzania ambaye ana ufaulu wakiwango chajuu .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni