Jumanne, 22 Julai 2014

.JESHI LAPOLISI NCHINI LAWASHIKILIA WANANE KWAKUTUPA VIUNGO VYA BINADAMU .

Timothy Marko.
KUFUTIA  kuwepo  kwa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini, juu ya kuzagaa kwa viungo vya mili ya Binadamu ikiwemo Vichwa ,miguu ,mikono,mioyo ,mifupa na mapafu naviungo vinginevyo vya binadamu huko Mbweni jijini Dar es salaam Jeshi lapolisi kanda maalumu ya jiji hilo  linawashikilia watu wanane waakiwemo madaktari ambao wanadaiwa kuhusikika kwa tukio hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini ,Kamishina wa jeshi lapolisi kanda maalum jijini Dar es salaam SULEIMAN KOVA amesema kuwa mnamo julai 27mwaka huu majira ya saa moja usiku jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa Raia wema ndipo jopo la wapelelezi wa jeshi hilo likaanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo likiongozwa na Mkuu wa polisi wa mkoa wakipolisi Kinondoni ACP CAMILLIUS WAMBURA .
‘’JOPO la polisi la upelelezi liligundua kuwa kulikuwepo na mifuko mieusi85 ambayo ndani yake kulikuwepo viungo vya Binadamu ikiwemo vichwa ,miguu,mikono ,Mioyo ,Mapafu ,Vifua pamoja na mifupa mbali mbali ya binadamu Viungo hivyo havikuwa navundo wala harufu nakuonekana kwamba vimekaushwa na kukakamaa.’’Alisema Kamishina Suleiman kova.
Kamishina Suleiman kova alisema kuwa katika eneo hilo pia jeshi hilo lilibaini kuwa kulikuwa navifaa vinavyotumika katika hospitali kama vile mipira yakuvaa mikononi,mifuko iliyotumika ,nguo maalumu ishirini pamoja na karatasi  mbili zenye maswali ya kujibu .
Alisema kuwa katika tukio hilo wananchi wasiopungua Elfu moja (1000)walifika katika eneo hilo lakini hakuna mwananchi aliyepatikana na taarifa sahihi nahatimaye viungo hivyo vika pelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi .
‘’Aidha jopo la wapelelezi chini ya Mkuu wa upelelezi kanda maalumu ACP JAFARI MOHAMED walianza  kufanya uchunguzi mara moja kwa kusaidiana na Daktari wa jeshi la polisi anaye husika nauchunguzi wa binadamu Forensic Doctor Ambaye walishirikiana namdakitari wa kutoka muhimbili ‘’Aliongeza Suleiman KOVA.
KOVA aliongeza kuwa Baada yauchunguzi huo ulibaini kwamba viungo hivyo kwa mara yamwisho vilikuwa kwenye maabara ya chuo kikuu cha madakitari IMTU jijini Dar es salaam,hatimaye jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata watu hao kwajili yauchunguzi zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni