Timothy Marko.
JESHI la polisi limefanikiwa kuwa kamata watu wawili ambao ni majambazi kufuatia majambazi hao kufanya jaribio la kumpora fedha mtu moja ambayejinalake halijafahamika bado katika benki ya NMB tawi la uwanja wa ndege jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini leo ,kamishina wa kanda maalumu jijini Dar es salaam Suleimani Kova amesema kuwa majambazi hao wakiwa na pikipiki aina ya boxer walimvizia mteja wa benki hiyo wakati akichukua fedha ili wamnyanga’nye fedha hizo kwa kutumia silaha mara atakapo toka.
‘’majambazi hawa walikamatwa baada yakufanya jaribio ya kumpora fedha aliyekuwa mteja wa benki ya NMB katika tawi la uwanja wa ndege ambapo majambazi hao walikuwa zaidi ya watatu walifanya jaribio hilo iliwamyanga’nye mteja huyo kwa kutumia silaha pindi atakapo toka kwenye benki hiyo’’Alisema Kamanda Sulemani kova .
Kamanda Suleiman kova alisema kuwa kufuatia jeshi lapolisi kupata tarifa ya msiri ambapo msiri huyo alitoa taarifa kwajeshi hilo kuwa benki hiyo kuwa kuna watu ambao wanapikipiki wanamvizia mteja huyo wa benki hiyo ya NMB ndipo polisi waliweka mtego kaika benki hiyo lakini majambazi hao walifanikiwakuimbia ndipo jeshi hilo lapolisi kwakushirikiana wananchi waliamua kuwakimbiza ndipo jambazi moja aliamua kufyatua Risasi lakini hatahivyo jeshi lapolisi lilipambana na majambazi hao nakuamua kufyatua risasi juu na kuwamuru majambazi hao wasimame.
Alisema kwa kushirikiana wananchi walifanikiwa kumkamata jambazi moja ambaye alikutwa nabastola moja aina ya Browing yenye namba za usajili namba 230787iliyoteng’ezwa katika nchi ya Szcheksolvakia ikiwa na risasi tatu hata hivyo kundi la wananchi wenye hasira kali waliendele akumshambulia jambazi huyo kwakutumia mawe lakini polisi walifanikiwa kumuokoa nahatimaye kumkimbiza hosipitali lakini jambazi huyo alifariki njiani ambapo jambazi huyo alikutwa naleseni ya udereva Daraja A,B,C,Eiliyotolewa 6october mwakajana kwa jina la Robert Gisegeti Nainai.
Katika hatua nyingine ,jeshi hilo kanda maalum jijini Dar es salam limetoa tahadhari kwa wananchi wajiji hilo kwa wafanyabiashara na wateja mbali mbali wa mabenki pamoja na taasisi za kiserikali nazile binafsi kuachana natabia ya kusafirisha fedha kwakutumia mifuko ya plastiki,kubeba fedha kwanjia yapikipiki nakubeba fedha hizo kwenye magari bila taadhari .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni