Timothy Marko.
Kitengo cha Damu salama nchini kwa kushirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jamii kimetoa hamasa kwa wananchi katika kuchangia damu kwajili ya wagonjwa wenye upungufu wa damu hususan wanawake nawatoto ambao ndio wahanga wa tatizo hilo.
Akizungumza jijini leo ,waziri wa afya naustawi jamii Dk.Self Rashidi amesema kuwa mpango huo nikufuatia maadhimisho ya siku yadamu salama duniani ambapo maadhimisho hayo kitaifa yanatarajiwa june 14 mwaka huu katika mkoa wa kigoma ambapo kauli mbiu ya madhimisho hayo ni changia damu okoa maisha ya mama namtoto.
‘’Mpango huu wa damu salama unalenga katika kuokoa maisha ya mama namtoto ambapo maadhimisho yamwaka huu yanatarajiwa kufanyika mkoani kigoma juni 14 mwakahuu yakiwa nakauli mbiu changia damu salama okoa maisha yamama namtoto’’Alisema DK Self Rashid.
Dk Self Rashid alisema maadhimisho hayo yatahudhuriwa na mke wa Rais wajamuhuri ya Tanzania mama Salma kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi inayojishughulisha namaswala ya wanawake hapa nchini ya (WAMA).
Alisema kumekuwepo nakundi kubwa la kina mama ambao hupoteza maisha kutokana nakukosa damu hapa nchini hivyo jamii inapaswa kuchangia damu ilikuhakikisha maisha ya mama namtoto hayapotei pindi wakati waujauzito.
‘’Maelfu ya wakina mama wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na upungufu wadamu hivyo jamii inapaswa kuchangia damu ilikuhakikisha maisha ya mama na mtoto hayapotei’’Aliongeza Waziri wa afya na ustawi wa jamii.
Aliongeza kuwa anatoa raikwa wananchi kuweza kuchangia damu ilikuweza kuokoa vizazi vijavyo pamoja na wanawake ambao ndio wamekuwa ni wa athirika janga hilo.
‘’natoa wito wananchi waweze kuchangia damu ilikuweza kuokoa maisha mama namtoto kwa vizazi vijavyo’’aliongeza waziri waafya.
Katika kupambana nawatumishi wasekta yaafya wasio waadilifu waziri wa afya na ustawi wajami Dk Seif Rashid ametoa angalizo kwa watumishi wa sekta ya afya wanaouza damu kinyemela kwa wagonjwa kuwa serikali haitosita kumchukulia mtumishi wasekta hiyo anayeuza damu kwa wagonjwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni