Jumatano, 21 Mei 2014

WLAC YAZINDUA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA KWA NJIA YASIMU KWA WANANCHI

Timothy  Marko.
Kituo cha msaada wa sheria kwa  wanawake nchini (WLAC)kimezindua  huduma ya msaada wakisheria kwa wananchi kwanjia ya simu katika kuhakikisha jamii yakitanzania inafikiwa na huduma  ya msaadahuo  bure.
Akizindua hudumahiyo jaji wa mahakama ya rufani ya Tanzania  Euserbia  Munuo amesema kuwa jamii imekuwa na uelewa duni wa maswala yahusianayo na sheria hali inayotokana na baadhi yajamii hizo kukosa kipato cha kukidhi maswala ya husianayo na msaada wa kisheria .
‘’jamii imekuwa ikikosa kupata msaada wa kisheria hii nikutokana nakuwa na uelewa duni wa maswala ya husianayo  na sheria  napia kutokuwepo kwa kipato kinachotosheleza  mahitaji ya maswala ya kisheria.’’alisema Eusebia  Munuo.
Jaji Eusebia Munuo alisema wanasheria wengi wahapa nchini wamekuwa huduma hiyo kwa Gharama kubwa hali inayopelekea wananchi wengi kukosa msaada wa huo wa kisheria.
Alisema uzinduzi wa namba ya 080078100 kwa msaada  wa kisheria hapa nchini  kwa kituo cha WLAC kutaweza kutatua changamoto yahuduma yakisheria hapa nchini .
‘’uzinduzi wa namba hii 080078100 utaweza kutatatua changamoto  za huduma ya msaada wa kisheria ambao wananchi wengi wamekuwa wakiuhitaji kwa muda mrefu’’alisema Munuo.
Mkurugezi mtendaji wakituo cha msaada wakisheria  kwa  wanawake (WLAC)Tenisiamuhulo alisema kuwa kituo hicho kinafanya utetezi wa maswala  yakisheria kwa wanawake na watoto.
Tenisia Muhulo alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 2006 kilianza kutoa hudumatofauti tofauti kwa njia ya simu kwa makampuni mbalimbali ikiwemo Tigo na aitel ambapo tualianza namba tofauti tofauti  ndipo tukauona umuhimu wa kuboresha namba ambayo ni0800780100.
‘’hapo mwanzoni tulikuwa tunatumia mitandao tofauti na namba tofauti katika mitandao yasimu  ya airtel na tigo lakini tukaonelea kufanya maboresho ya namba za msaada wa kisheria ilkuwafikia watu wengi’’alisema Muhulo.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni