Timothy Marko.
Imebanika kuwa kumekuwa na ukiwakwaji wasera ya afya katika hospitali zinazo milikiwa na serikali katika utoaji wa huduma za afya kwa baadhi ya makundi yawazee na watoto,hali inayopelekea kutozwa fedha kwa makundi hayo ikiwa nikinyume cha sheria zinazo mtaka mtoa huduma kulihudumia kundi hilo bure bila kutozwa fedha.
Hayo yamebaishwa leo na taasisi isiyokuwa yakiserikali ya TWaweza katika semina iliyoandaliwa nataasisi hiyo wakati ikizinduamatokeo ya ripoti inayoanisha hali ya sekta yaafya katika hospitali za serikali katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa matokeo hayo yatafiti yaliyofanywa na kituo hicho mtafiti wa twaweza Elvis Mushi amesema kuwa zaidi ya asilimia77 yawananchi hutembelea vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali huku kumekuwa tabia kwa baadhi yawauguzi katika sekta hiyo kuwatoza huduma ambazo hupatiwa bure kwabaadhi yamakundi kwa baadhi yawazee nawatoto.
‘’kutokana naupungufu wa wauguzi katika hospitali za serikali baadhi ya waaguzi katika hospitali za serikali huwatoza fedha ilikuweza kupata huduma ya matibabu ikilinganishwa na vituo vya afya vinavyomilikiwa na taasisi au sekta binafsi ‘’alisema Elvis Mushi.
Elvis Mushi alisema kuwa baadhi yawagonjwa wengi waliopo hutembea zaidi ya dakika 30 ilikuweza kupata huduma hiyo ya afya hususan maeneo yavijijini .
Katika hatua nyingine mtafiti huyo amamebainisha kuwa baadhi ya wagonjwa hunyimwa haki yao ikiwemo haki yakupata huduma za afya kikamilifu kutokana nakukosa madawa pindi waaendapo katika hosipitali za serikali.
Kwa upande wake mkuu wa taasisi hiyo ya twaweza Rakesh Rajani amesema kundi la wazee nawatoto limekuwa likipatashida katika kupata huduma za afya kutokana kutokana na sera zisizotekelezeka kuhusiana nakundi hilo katika kupata matibabu .
‘’wazee nawatoto wanaumia kwa sababu yakuwepo kwa sera zisizo tekelezeka maranyingi kumekuwa namaneno matupu serikali inahitaji kutimiza wajibu wake kwakuwatunuku wanaotoa huduma vizuri nakuwa wajibisha wanaotoa huduuma vizuri’’alisema Rakeshi Rajabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni