Timothy Marko.
Mkazi mmoja jijini amekufa maji kufuatia mvua zilizonyesha hivi karibuni nakusababisha maafa kwa nyumba nyingi za jijini .
Akitoa taarifa kamanda wa jeshi lapolisi wa kanda maalumu jijini Dar es salaam suilemani kova alisema tukio hilio lilitokea 30march mwaka huu majira ya saatatu nanusu asubuhi .
Aidha kamanda kova alimtaja mtoto huyo idd Mohamed ( 14) mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari msechule iliyopo jijini nakuongeza kuwa mtoto huyo alikutwa akiwemo kwenye mto msimbazi akiwa amefariki dunia.
‘’maiti yamtoto huyo iliopolewa na askari wa kikosi cha zimamoto cha uokoaji chajiji wakisaidiana na wakaazi wa eneo hilo hata hivyo mwili wake ulikutwa umeshaharibika ‘’alisema kamanda suileman kova .
Kamanda kova alisema enzi za uhai wake mtoto huyo march 29 mwaka huu alishwahi kukumbwa lakuzolewa namaji katika mto huo huo wa msimbazi akanusurika.
Alisema maiti ya mtoto huyo imehifadhiwa ilikuweza kufanyiwa uchunguzi wa kidakitari.
Katika hatua nyingine kamanda kova alisema mnamo 30 march mwaka huu majira ya saa saba nanusu mchana katika eneo la vingunguti kata ya mnyamani katika wilaya ilala gari lenye namba za usajili T556 BHQ aina ya Toyota costal ikiendeshwa na mpangala (37)mkazi wa vingunguti buguruni ameweza kusababisha ajari nakusababisha kifo cha mtu moja .
Alisema mwili wamahiti huyo imeifadhiwa katika hospitali ya amana nakuongeza kuwa dereva aliyesababisha kifo hicho ana shikiliwa na polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni