Msajili wa vyama vya siasa Francis Mutungi |
Msajili wa vyama vya Siasa nchini Jaji Francisis Mutungi leo amevifutia usajili vyama vitatu ikiwemo chama cha haki na ustawi (Chausta) African progress Party pamoja na Chama cha Jahazi Asilia .
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es salaam Jaji Mutungi amesema kuwa hatua yakuvifutia usajili vyama hivyo imetokana na vyama hivyo kukiuka masharti ya usajili na kutokamilisha matakwa yakisheria pamoja nazoezi la uhakiki ambalo lilifanyika juni 26 hadi julai26 mwaka huu.
''Katika zoezi letu la uhakiki ilibainika kuwa vyama vya Jahazi na CHAUSTA viliipoteza sifa zakuwa msajili wa kudumu na kuitwa katika ofisi yamsajili kwanini havijakidhi vigezo hivyo nakushindwa kujitetea ''Alisema Jaji Francis Mutungi .
JAJI Mtungi alisema kuwa moja ya sifa ambazo vyama hivyo vilipoteza nakutokuwa nausajili wakudumu nipamoja kutokuwa na ofisi ya chama Tanzania bara kwa mujibu wakifungu 10(d) pamoja na kutokuwa na wanachama wake zanzibar kwamujibu wa wakifungu cha 10 (B)
Alisema vigezo vingine nipamoja na kushindwa kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya mwaka kwa mtibiti na mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali iliziweze kukaguliwa kwamujibu wakifungu 14(1)b(I) .
''Vigezo vingine nipamoja kushindwa kuwasilisha kwamsajili wa vyama vyasiasa tamko la orodha ya mali za chama kwamujibu wakifungu cha 14(1)(b)(II) aidha vigezo vingine nipamoja na kushinndwa kutekeleza matakwa ya kifungu cha 15(1)kwamba mapato yote yafedha ya chama yawekwe kwenye akaunti ya chama ''Aliongeza Jaji Franciss Mutungi .
Mutungi alisema kutokana na vifungu 7(3)cha sheria ya vyama vyasiasa taasisi yoyote hairusiwi kufanya kazi kama chama chasiasa kama hakijasajiliwa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni