NA HASSAN
SILAYO-MAELEZO
Wakuu wa
Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kuweka kuweka mazingira
wezeshi kwa
wawekezaji nchini ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa
ajili ya
ujenzi wa viwanda nchini.
Akizungumza
wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha
kutengeneza
vifungashio kilichopo wilayani Kihaba mkoani Pwani Katibu
Mkuu Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru
amesema kuwa
tukiwa tunaelekea katika nchi ya viwanda serikali
inajukumu la
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji nchini.
Dkt.
Adelhelm amesema kuwa viongozi hao hawana budi kuiga mfano wa
Mkuu wa Mkoa
wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa ushirikiano
wanaoutoa
kwa wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi
wa viwanda
katika mkoa huo.
“Dhumuni la
serikali kwa sasa ni kuhakikisha tunaifikia nchi ya uchumi wa
kati kupitia
viwanda,na hili tutalitekeleza pia kwa kushirikiana na sekta
binafsi na
ni jukumu la viongozi ikiwemo wakuu wa wilaya na wakuu wa
mikoa nchini
kote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji ikiwemo
kutenga
maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda”. Alisema Dkt. Adelhelm
Dkt.
Adelhelm aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2020 Serikali
imepanga
kuhakikisha sekta ya viwanda nchini inachangia asilimia 15
kwenye pato
la taifa kutoka asilimia 7.3 iliyopo hivi sasa.
Pia Dkt.
Adelhelm alisema kuwa Serikali imepanga kuongeza idadi ya ajira
za viwandani
na ajira zitokanazo na sekta ya viwanda hadi kufikia asilimia
40 ifikapo
mwaka 2020.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) Bw. Mlingi
Mkucha
amesema kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni