Timothy
Marko.
KIWANGO cha
Mauzo yahisa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE)kimeongezeka kutoka
shilingi bilioni 16.2 hadi kufikia shilingi bilioni 19.4 kwa wiki hii ambapo
ongezeko hilo ni sawa na asilimia hamsini
ya mauzo yaliyopita .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa Mwandamizi wa Soko hilo Mary
Kinabo amesema kuwa wakati kiwango chamauzo yahisa kikipanda na kufikia shilingi bilioni 19.4 idadi za hisa
zilizouzwa na kununuliwa zimeshuka kwa asilimia 50 hadi kufikia hisa milioni
2.4 ikilinganishwa na hisa 4.8 za awali.
‘’Ukubwa
wamtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 0.05 kutoka shilingi trioni 21.58 hadi
trioni 21.57 wakati makapuni yanayo ongoza kwa idadi za hisa kuuzwa na kunuliwa
nipamoja na TBL(58%) ,CRDB(32%) wakati Soko lahisa la Dar es salaam lishika
nafasi ya tatu kwa asilimia nne kwa idadi yahisa za kuuzwa na kunuliwa ‘’Amesema
Afisa Mwandamizi Mary Kinabo .
Afisa
Mwandamizi Kinabo amesema kuwa wakati ukubwa wa mtaji wa makapuni yandani
ukipungua kwa asilimia 0.29 sekta ya viwanda katika wiki hii imeonesha kupanda
kwa pointi 48.77baada ya bei ya hisa za TBL Kupanda kwa asilimia 1.56
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni