Jumatatu, 3 Oktoba 2016

SERIKALI YAZITAKA JUMUHIA ZA KIMATAIFA KUENDELEA KUTOA MISADA ZAIDI MKOANI KAGERA .



Timothy Marko.
SERIKALI imewataka wahisani mbali mbali  kuweza kutoa michango mbalimbali ilikuweza kuwasaidia wahanga watetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni .

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la uwezeshaji wa mifuko ya jamii jijini Dar es salaam Katibu Mkuu ofisi ya Rais Peter ilomo amesema hadi hivi sasa tetemeko hilo  watu ishirini wamepoteza maisha yao ,huku jumla ya nyumba takribani 7840 zimeweza kuharibiwa natetemeko hilo .

‘’Ninaziomba taasisi najumuhia mbalimbali za kimataifa kuweza kutuchangia kupitia mfuko wa majanga ilikuweza kufanya marekebisho ya sehemu zilizo haribiwa ‘’Alisema Katibu Mkuu Peter Ilomo .

Katibu Mkuu ofisi ya Rais Ilomo amesema kuwa kupitia mfuko huo wa majanga serikali itaweza kufanyatathimini kwa kufanya utafiti mblimbali ilikuwezesha mpango wa mfuko huo  kuweza kufikia malengo yake .

Alisema kuwa takribani vijiji 9976  vimeweza kua athiriwa natekemeko hilo ambapo watu jumla milioni 1.1 walioathiriwa na tetemeko hilo wahitaji kiasi cha shilingi bilioni 623 ilikuwezesha mfuko huo wamajanga kuweza kufanya kazi ipasavyo .

‘’Habari njema kutokana makubaliano na wahisani ambapo mkataba wake ulisainiwa june mwaka huu ni hatua nzuri za kuunganisha nguvu ilikuweza kufanya kazi vizuri ilkuweza kutunisha mfuko huu wa majanga hii ni hatua nzuri yakuuboresha mfuko huu ‘’Aliongeza ilomo .

KATIBU Mkuu aliyataka mashirika yakimataifa ikiwemo benki yadunia ,DFID SIDA ,UNDP ,UNICEF ILO pamoja UNFPA  kuzidi kushirikiana naserikali ya awamu yatano katika mipango ya maendeleo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni