MKURUGENZI WA TAASISI YA TWAWEZA IDAN LYAKUZE AKITOA TAARIFA YA UTAFITI JUU YA UWEZO WANAFUNZI WANAOJUA KUSOMA NA KUANDIKA KATIKA SHULE ZA MSINGI NCHINI. |
Timothy
Marko
IMELEZWA kuwa baadhi ya wanafunzi wa darasa
la saba hawawezi kufanya majaribio ya darasa la pili ambapo wanafunzi Wanne kati ya kumi sawa na asilimia 44 walipo shule
za msingi za serikali hawawezi kusoma hadithi ya kingereza ya kiwango cha
darasa la pili ambapo wanafunzi wawili kati kumi sawa na asilimia 16 hawezi
kusoma hadithi ya kiswahili ya kiwango cha darasa la pili huku wanafunzi wawili
kati ya kumi sawa na asiimia 23 hawawezi kufanya hesabu za kuzidisha za kiwango
cha darasa hilo.
Utafiti
ulifanywa na twaweza ulionesha kuwa pamoja nakiwango hicho, familia ambazo zinauwezo mkubwa wa kiuchumi
hasa zile zinazoishi mijini zinauwezekano mkubwa zaidi wa kupata stadi za
msingi za kusoma na kufanya hesabu.
Aidha,
ulieleza kuwa katika masomo yaliyotolewa tathimini juu ya uelewa wa wanafunzi
katika shule hizo, ulionesha kuwa katika masomo matatu ya kingereza na Kiswahili
na hesabu ulibainisha ni asilimia 19 ya wanafunzi washule yamsingi waliweza
kusoma kingereza .
Ulibainisha kuwa
katika takwimu zilizopo kati ya wanafunzi walipo katika shulehizo niasilimia 23
ya wanafunzi walitoka katika kaya
masikini wakati kaya 62 wanatoka katika kaya zenye uwezo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni