Timothy
Marko.
BENKI ya
kibiashara ya NMB imeingia makubaliano na Wakala wa usajili wa Makampuni (BRELA) katika malipo ya
usajili wa makampuni kupitia benki hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha
mihamala wa benki hiyo Michaeli Mungure amesema kuwa malipo hayo yausajili wa
makampuni yatakuwa katika mifumo mbalimbali ya malipo ikiwemo mfumo wa Nmb
Mobile ulioanzishwa na benki hiyo .
‘’Kupitia
Makubaliano tunayo yafanya hii leo na Wakala wa usajili wa makampuni
(BRELA)huduma ya tozo za usajili wa makampuni kupitia NMB mobile hii ninjia
rahisi itakayo muwezesha Mameneja Wa makampuni kulipa ada za usajili kupitia
mifumo yakibenki ikiwemo NMBmobile ‘’Alisema Mkuu wa Kitengo cha Mihamala
Michael Mungure .
Mkuu wa
kitengo cha Mihamala NMB Mungure alisema kuwa huduma hiyo imeshakamilika
ikiwemo mifumo ya taasisi hiyo itakayo wawezesha makampuni kuweza kulipa
mihamala yao kwa wakati .
KATIKA hatua
nyingine Kaimu Meneja wa Wakala wa Usajili wa Makampuni BRELA Bosco Gadi amesema
kuwa benki ya NMB ni benki ya kwanza inayodumisha ushirikiano na taasisi hiyo .
Bosco Gadi
amesema kuwa taasisi yake inajishughulisha na usajili wa viwanda na majina
mbalimbali ya Biashara ikiwemo kusajili
makampuni kupitia tozo mbalimbali za usajili wa makampuni .
‘’Hii
nifursa nzuri ya kurasimisha biashara na kupunguza gharama za kulipa ada ‘’Alisema
Gadi .
Gadi alisema
kuwa hii nihatua nzuri itakayo wawezesha wafanya biashara kurasimisha biashara
zao nakuiwezesha serikali kuweza kupata mapato na kukuza uchumi wataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni