Kamishina wa Kanda Maalum Dar es salaam. SIMON SIRRO |
KAMISHINA wa Polisi Kanda Maalum (CP) Simoni Sirro amekitaka Chama cha demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA)Kudumisha amani na utulivu nakuendelea kuwa wazalendo ilikuweza kukuza maendeleo yakiuchumi nchini .
Akizungumza na wandishi wahabari jijini Dar es salaam Simon Sirro amesema hatua yakusitisha maandamano yaliyotakiwa kufanyika kesho nikitendo cha kiungwana na hali hiyo inaonesha chama hicho niwazalendo kwa nchi yao .
''Hatua ya chadema kusitisha Mandamano yaliyotakiwa kufanyika kesho nikitendo cha kiungwana na ni cha kizalendo hivyo ninawasihii wanachama wachadema kuzidi kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao ilikuweza kuleta maendeleo yakiuchumi ''Alisema Kamishina Simoni Sirro .
Kamishina Sirro alisema sambamba nahatua ya Chadema kusitisha Maandamano yaliyotakiwa kufanyika kesho nchi nzima ,jeshi hilo limesema litaendelea kufanya patrol katika viunga vyote vya jiji la Dar es salaam ilikuzuia vitendo vya kihalifu vitakavyojitokeza .
Alisema Jeshi hilo bado linawataka viongozi wa chama hicho kuendelea kuripoti katika makao makuu yajeshi hilo jijini Dar es salaam, hata hivyo jeshi hilo bado linaendelea nauchunguzi wa mauaji ya polisi yaliyofanyika huko vikindu jijini Dar es salaam .
''Mbaka sasa tunawashikilia watuhumiwa ishirini waliohusika na mauaji ya askari polisi huko vikindu lakini tunaendelea naupelelezi zaidi juu ya mauaji huko vikindu nataka kuwa hakikishia kuwa Dar es salaam ipo shwari ''Aliongeza Kamishina SIRRO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni