Jumanne, 31 Mei 2016

SEKETARIETI YA AJIRA YAWATAKA WAOMBAJI KUTUMIA SAYANSI NATEKNOLOJIA KATIKA KUTAFUTA NAFASI ZA AJIRA.



Timothy Marko.
SEKTERARIETI ya Ajira imewataka waombaji wa ajira nchini kuweza kutumia mifumo ya kietroniki ijulikanayo kama (recruitment Portal )ilkuweza kupunguza muda wakujibiwa maombi yakazi katika ofisi wanazotumia kuomba nafasi za ajira .

Akizungumza na waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkuu wakitengo cha Mawasiliano serikalini katika taasisi hiyo Riziki Abraham amesema kuwa mfumo huo umeweza kupunguza siku za uendeshaji wa mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi kufikia 52 .

‘’Mfumo huu umeweza kuwasaidia waombaji wakazi kuwa na uhakika wa maombi yao kupokelewa kwa wakati nakupata mrejesho wapapo kwapapo tofauti nailivyokuwa awali ambapo maombi yakazi yalikuwa yakipokelewa ‘’Alisema Mkuu wakitengo cha Mawasiliano Riziki Abraham.

Riziki Abraham alisema kuwa kufuatia kutumia mfumo simu kiganjani umeweza kuongeza idadi ya waombaji ajira nakurahisisha taarifa zafursa za ajira nakuweza kuwafikia maeneo mengi zaidi ambapo muhusika anatakiwa kujisajili katika mifumo inayotangazwa na serikali .

Alisema Hadi kufikia Mei 29 mwaka huu jumla waombaji wafusra za ajira 97,765 waliweza kuandikishwa katika mfumo huo wakieletroniki kati yao waombaji 89,484 wameweza kupata fusra za ajira kwakutumia simu za viganjani .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni