MWANAHARAKATI KWANZA BLOG

Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.

Jumatatu, 20 Juni 2016

MULTIPLE CHOICE TANZANIA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KWA KUVIENDELEZA VIPAJI VYAO.

Conversation opened. 2 messages. All messages read.

Timothy Marko.

KATIKA kuhakukisha sekta ya biashara inakuwa hapa nchini kampuni ya multiple choice Tanzania imemuteuwa Mkurugenzi Maharage Chande kuwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo.

Akizungumza katika uteuzi huo Mkurugenzi wa kampuni yaw a mutiplechoice Maharage Chande amesema kuwa  kuteuliwa kwake kunafuatia hatua ya kampuni hiyo katika kuboresha raslimali watu wa kampuni hiyo inayoongoza hapa  nchini.
‘’Kampuni hii ya multiple choice inalenga kukuza  kampuni ya multiple choice kwa kuwajili watu wenye uwezo ikwemo wenye ujuzi mbalimbali ili kuweza kuakikisha kampuni hii inakuwa kibiashara’’ Alisema Maharage Chande.

Mkurugenzi Maharage Chande alisema kuwa katika kufanikisha jukumu hilo kampuni ya multiple choice imeamua kuwekeza kwa kuinua na kuboresha rasilimari watu kwa kuwaongezea ujuzi mbalimbali ili kuleta matokeo bora ya kampuni.

Alisema kuwa kutokana na kampuni ya multiple choice Tanzania kutambua umuhimu wa kukuza raslimali watu kampuni hiyo imekuwa bora katika ukanda wa kusini mwa afrika pamoja na dunia kwa ujumla katika huduma mbalimbali za kuburudisha na kuelimisha jamii kupitia chaneli zake barani afrika.

‘’Kampuni hii ya multiple choice imekuwa ni bora barani afrika baada ya kutambua vipaji mbalimbali  vya raslimali watu walioajiliwa katika kampuni na kuweza kuviendeleza ili kuweza kuleta matokeo bora katika  kampuni ‘’Aliongeza  Mkurugenzi Chande.






Recent photos
View photo in message
Show details

Press Release - MCT Announcement (2).docx
Displaying Press Release - MCT Announcement (2).docx.
Unknown kwa 07:34
Shiriki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

‹
›
Nyumbani
Ona toleo la wavuti
Inaendeshwa na Blogger.