Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumanne, 21 Juni 2016
SSRA YAPANGA KUWAFIKIA MAMALISHE NA BODA BODA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU .
Timothy Marko
MAMLAKA ya uthibiti wa mifuko yahifadhi yajamii nchini (SSRA)imewataka wananchi kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii ilkuweza kupata huduma za matibabu ikiwemo kupatiwa bima ya afya .
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugezi wa mamlaka ya udhibiti wa mifuko yahifadhi yajamii SSRA Ali Masaninga amesema hapo awali mifuko hiyo ilijikita katika sekta iliyorasmi hali ambayo imechangia kuacha kundi kubwa la wananchi wasio kuwa katika sektahiyo kukosa huduma yahifadhi yajamii ikiwemo bima ya afya.
''Kwakuona umuhimu wa mifuko yahifadhi yajamii kwa sekta iliyorasmi katika kupata huduma za mafao yamatibabu kwa kutumia bima ya afya ,tumegundua kuwa mbeleyetu tumeliacha kundikubwa la wananchi ambao hawapo katika sekta isiyorasmi ambao wanataka kujiunga na huduma yabima yaafya''Alisema Ali Masaninga .
Mkurugenzi Masaninga alisema kuwa kwakutambua uhitaji mkubwa wa bima ya afya kwa wananchi mamlaka hiyo yaudhiti wamifuko ya hifadhi ya jamii imeamua kulilenga kundi la wafanyabishara wadogo wadogo ikiwemo madereva wa bodaboda pamoja mamalishe ilkuweza kufikia kundi hilo kwenye hifadhi yajamii na bima yaafya kwa ujumla .
''Progamu hii imeshaanza kwa wilaya 27 ambapo tumeanza namikoa ya kanda yakati nakusini ''Aliongeza Masaninga .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni