Timothy
Marko.
KATIKA
kuhakikisha sekta kilimo inakuwa hapa nchini Shirika lisilo lakiserikali la
Fund For Rural prosperity limeanzisha miradi ya mikopo katika kuwasaidia
wakulima wadogo ili kuwawezesha kiuchumi na kuondokana na hali ya umasikini.
Mikopo yenye
thamani ya dola za kimarekani milioni35 fedha hizo zitagawiwa katika vikundi
vya akiba vinavyojishughulisha nakilimo walipo katika kaya masikini zilizopo
vijijini katikanchi za bara la afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mshauri wa taasisi hiyo Gabriel Kivuti amesema kuwa
kwakushirikiana na taasisi zakifedha zilizopo hapa nchini taasisi hiyo imeamua
kutoa fedha ambazo sio za mkopo ilikuweza kumsaidia kiuchumi mkulima
mdogomdogo.
‘’Katika
kipindi cha mwaka jana taasisi yetu imetoa zaidi yadola zakimarekani milioni 35
ikiwa nalengo lakuwasaidia wakulima wadogo wawadogo mradi huu wa mfuko kwa jili
yamaendeleo vijijini unasimamiwa na Taasisi ya KPMG international Development
advisor services Afrika ‘’Alisema Mshauri Gabriel KIVUTI .
Mshauri
Kivuti alisema kuwa kumekuwepo na changamoto nyingi katika kaya nyingi zilizopo
vijijini barani afrika kutoshirikishwa katika masuala yakifedha ambapo zaidi ya
asilimia 70 kaya masikini zilizokusini
mwajangwa la sahara zimekuwa zikitegemea kilimo kama uti wa mgongo wauchumi .
Alisema
wakulima wadogo wadogo wamekuwa wakikabiliwa nachangamoto ya baadhi ya taasisi
za kifedha kuweza kuwafikia katika maeneo yao hali inayozorotesha jitihada za
kukwamua sekta yakilimo na wakulima wenyewe.
‘’Gharama
kubwa zakufanya biashara ,ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi namiundo mbinu
yabiashara isiyo badilika inazorotesha jitihada za kupanua bidhaa sahihi ambazo
zingeweza kuwasaidia kaya masikini’’Aliongeza KIVUTI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni