Timothy Marko.
WAFANYAKAZI
wa ujenzi wajengo la Mwalimu Nyerere(CRJ) SQUIRE wamemlalamikia mkandarasi wa jengo
hilo kwa kutowalipa stahiki zao kwa wakati nawakati huo huo wamemlalamikia
mkandarasi huyo kwakuwalipa shilingi 5000 kwasiku hali inayofanya wafanyakazi
hao kutokidhi mahitaji yao
.
HAYATI MWALIMU NYERERE |
‘’Tatizo la
msingi ndugu mwandishi nibaada ya taarifa ya wizara ya ajira kuwataka wajiri
wote watoe mikataba kwa wafanyakazi wao ,tunachokihitaji sisi hapa nikupewa
mikataba yetu ya ajira inayozingatia
vigezo vyote vya mkataba ‘’Alisema Kelvin Roman .
Kelvin
alisema kuwa hivi karibuni waziri wa ujenzi profesa Makame Mbarawa alitaka katika
sekta ya ujenzi wafanyakazi wote wapewe mikataba .
Alisema kuwa
wamepewa mikataba ambayo haioneshi lini wafanyakazi hao walianza kazi
nakusisitiza kuwa mikataba hiyo imekuwa ikitolewa kwa kificho kwa baadhi ya
wafanyakazi
‘’Mikataba
haioneshi lini mfanyakzi alianza kazi ,nawala mkataba huu unasema utalipwa
kwawiki hali inayo changia sitofahamu na ajira zetu ‘’Alisema Kelvin Roman.
Meneja
Rasmali watu wa kampuni ya CRJ anaye jenga jengo hilo Tatina Yang amesema kuwa
ameweza kufuata maelekezo yaserikali lakini kinachosekana katika kampuni yake
ni uelewa mdogo wa masuala ya mikataba katika makampuni .
Alisema kuwa
kinachofuata sasa nikuwasikiliza matatizo yao ili tuweze kuweza kuyatatua kwa
kusanya maoni yao.
‘’Kama
kampuni hii itafungwa wafanyakazi watakosa ajira na watu hawa hawatakidhi
mahitaji yao ‘’Alisema Yang.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni