Jumanne, 16 Februari 2016

WAZIRI WAELIMU NCHINI AMTUMBUA JIPU MKURUGENZI WA BODI YAMIKOPO(HELB)



Timothy Marko.
WAZIRI wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini Jocyce Njalichako amemuondoa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo George Nyatega baada ya kutotoa mikopo ya wanafunzi kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam waziri Njalichako amesema kuwa wanafunzi 23 waliweza kupata mikopo katika vyuo viwili tofauti kwa kipindo cha miaka mitatu mfululizo .
"jumla ya sh 153,999,590 ambazo zililipwa kwa chuo cha kwanza wakati huohuo chuo cha pili kilipwa sh 147,541,460 katika ya wanafunzi 169" alisema Njalichako

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YAUFUNDI STADI JOYCE NDALICHAKO .

WAZIRI Njalichako alisema kuwa jumla ya wanafunzi 343 wasiokuwa na usajiri kwenye vyuo husika waliweza kulipwa jumla ya sh 342,468,500 wakati huohuo wanafunzi 55 walioacha masomo walilipa kumla ya sh 136,232,800.

Alisema kuwa takribani jumla ya sh 159,664,500 zililipwa kwa wanafunzi 306 ambao ni kiwango kilichobainishwa kwenye vipengere namba 4 .3 na 4.3.2 cha miongozo ya ukopeshaji wa mwaka 2008,2009.

" kwa mujibu wa kifungu D.5(3) cha kanuni za kudumu kinachohusu uteuzi wa maofisa wa serikali pamoja na kifungu D 12 kinachohusu taarifa za mtendaji na kifungu f.50(1) kinachohusu usitishaji wa mkataba kwako mawaziri nimemsitisha mkataba wa ajira bw George Nyatega kama mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo" aliongeza 

WAZIRI Ndalichako katika hatua nyingine amewasimamisha Yusuphu Kisela ambaye no mkurugenzi wa fedha na utawala, Juma Changoja ambaye ni Mkurugezi wa uwezeshaji mikopo pia amsitisha Onesmo Laiza ambaye no mkurugenzi wa upangaji na utoaji mikopo wa bodies hiyo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni