Jumatano, 3 Februari 2016

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUPIMA SARATANI






Timothy Marko .
SERIKALI imewataka wananchi kuweza kujitokeza katika vituo vya afya  kupimwa satarani ili kuweza kufanyiwa uchunguzi  wa ugonjwa huo kabla ya madhara makubwa hayajajitokeza .

KATIBU MKUU wa wizara ya afya na ustawi wa jamii ULISUBISYA MPOKI

Wito huo umetolewa na Katibu mkuu  wa wizara ya afya Ulisubisya Mpoki wakati akizungumza nawaandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam juu yasiku kongamano maaluum la uelimishaji juu ya ugonjwa wa saratani ambapo amesema kuwa jumla yawagonjwa 44000 wameweza kugundulika na ugonjwa huo .
‘’Kati ya wagonjwa wa saratani asilimia 10 tu ndio hupimwa saratani nakugundulika na ugonjwa huu wakati huo huo asilimia 80 yawagonjwa hufika wakati wapo katika hatua yamwisho ya ugonjwa ‘’Alisema katibu mkuu Ulisubisya Mpoki.
Katibu mkuu Mpoki alisema kuwa katika takwimu zilizopo wanaume wamekuwa wakikumba na mataizo ya saratani yangozi ,satani tezi dume na wanawake wamekuwa nasaratani ya shingo yakizazi .
Alisema kuwa sababu zinazochngiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi wa saratani nikuwepo kwa tabiza mtindo wakimaisha ikiwemo ulevi ,uvutaji sigara na utumiaji wamionzi na miale ya mashine .
‘’Unene uliokithiri unaweza kusabisha saratani ,matumizi mengi yasukari nakutofanya mazoezi ,matumizi yapombe hali inachangia kuaharibika kwa mfumo wa fahamu ‘’Aliongeza katibu mkuu ulisubisya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni