JAJI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA . |
Timothy Marko.
JAJI Mkuu wa
mahakama kuu ya Tanzania Jaji Othman Chande ametoa siku saba kwa majaji wafawidhi kuchambua na kuanisha mahakimu wote
walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua nakufikia kesi 250
hadi kesi 260 kwa mwaka 2015,pamoja na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku
saba kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa.
Jaji Chande
alisema kuwa kiwango cha kesi kwa kila hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi na
mahakama ya wilaya ni 250,na mahakimu wakazi 121 kwenye mahakama za hakimu
mkazi na Mahakama za wilaya,wameamua
kesi chini ya 100 kwa mwaka 2015.
Aliongeza
kuwa kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ni 260,ambapo mahakimu
wakazi na mahakimu wa mahakama za mwanzo ni ni 387 wameamua kesi chini ya 100
kwa mwaka 2015.
Alifafunua
kuwa uchambuzi,uchunguzi wa mashtaka ya nidhamu ukiondoa wale ambao wameajiriwa
karibuni,wanaofanya kazi kwenye mahkama za mwanzo zisizokua na mashauri
mengi,au waliokwenda masomoni katikati ya mwak,au likizo za ujauzito.
Aidha
alisema mashtaka ya nidhamu kifungu cha 50 na 51 cha sheria ya uendeshaji wa
mahakama (judiciary administration act,namba 4 ya mwaka 2011 zimeanzisha kamati
za maadili za mahakimu za mikoa na wilaya.
Alitaja
kamati hizo ni kamati ndogo za tume ya utumishi wa mahakma iliyoundwa chini ya
ibara 112 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,mwaka 1977 kam mojawapo
ya majukumu yake kusimamia nidhamu na utendaji kazi mzuri wa mahakimu ibara 113
(1) E.
“mahakimu
wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoa sababu za
kuridhisha kwanini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa
watafunguliwa mashtaka ya nidhamu na mashtaka yatashughulikiwa haraka na kamati
za maadili za mahakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki’alisema
Alibainisha
kuwa uwajibikaji ni hatua muhimu katika mazingira ya sasa ambapo kuchapa kazi
na uwajibikaji ni kauli mbiu ya utumishi wa umma’ambapo katika mazingira hayo
mahakama ilianza maboresho na kufanya kazi kwa mikakati na malengo tangu mwaka
2013,mahakimu wasiofikia malengo wamekua kama nanga inayozuia jahazi letu
kufikia kule tunakotoka kulipeleka kwenye sifuri.
Hatahivyo
alisema kuwa mahakama haitavumilia hakimu yeyote anayebembeleza kesi,hivyo
hakimu haitakiwi kubembeleza kesi bali inatakiwa amalize kesi kwa wakati
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni