Timothy Marko.
SOKO la hisa
la Dar es salaam(DSE) limewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuweza
kushiriki katika shindano la scholar Investment Challenge ilikuweza kujipatia
fursa ya kuajiriwa katika taasisi za kifedha .
Akizungumza
Meneja Mauzo na Biashara wa soko hilo Partick Mmsusa amesema katika shindano
hilo linalotarajiwa kuanza mwezi April hadi juni mwaka huu litawezesha
wanafunzi wa vyuo wanaoshiriki shindano hilo kuweza kupewa mtaji unaotokana nauwekezaji
wa hisa kwa kununuahisa za makapuni mbalimbali zinazo uza hisa zake kupitia
soko hilo .
‘’Shindano
hili la Scholar Investment Challenge litawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuweza kupata
fursa ya kuajiriwa katika Taasisi za kifedha ikiwemo CRDB pamoja FDC ‘’Alisema
Patrick Mmsusa .
Meneja
Biashara Mmsusa alisema kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamekuwa
wakikabiliwa na changamoto ya ajira pindi wamalizapo masomo yao chuoni hivyo
kwakutumia fursa hiyo wataweza kuajiriwa nataasisi za kifedha nakujiajili
wenyewe .
Alisema
Mwanafunzi wachuo anaweza kujiunga nashindano hilo kwakutembelea tovuti ya soko
hilo ambayo ni info.dse.co.tz
‘’shindano
hili nila kila mwanafunzi aliye katika vyuo vikuu vinavyotambulika naserikali
,baada yashindano hili mwanafunzi atapata fursa mbalimbali zakujiliwa na
taasisi zakifedha’’Aliongeza Mmsusa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni