Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatano, 2 Desemba 2015
SERIKALI YA WATAKA WAZALISHAJI WA FILAMU KUZINGATIA MAADILI.
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha bidhaa za filamu zinakuwa na ubora wa kimataifa unaozingatia utamaduni wa mtanzania ,bodi ya filiamu nchini imesema kuwa, itaendelea kuzikagua filamu zinazoendelea kuzalishwahapa nchini, ikiwemo kuangalia vigezo mbambali vya uzalishaji wa filamu hizo wenye kuzingatia maadili .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Genofeva Matemu amesema kuwa viongozi wengi wakitaifa wamekuwa mstari wa mbele ilikuhakikisha tasinia hiyo inasonga mbele ikiwemo kuratibu na kusimamia usambazaji wa filamu nchini .
‘’kumekuwa na ukuajimkubwa wasoko lafilamu hapa nchini ikiwemo kusambaza kazi za filamu kwanjia yamtandao na kufanya Tanzania kusifika katika tasniahii ya filamu Serikali imechukua hatua madhubuti ikiwemo kurejesha nidhamu na kuendesha kihalali kwa kuweka mifumo ya kisheria na kurasimisha ‘’ Alisema Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Geno feva MATEMU .
Kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Genofeva alisema kuwa kutokana naumuhimu wa tansinia hiyo katika kukuza uchumi wa taifa kitengo hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kuratibu mafunzo ya watalamu wa zalishaji wa filamu kwakuwahusisha watalamu wan je na ndani na nje .
ALISEMA kuwa serikali inawahamasisha wadau mbalimbali wa sekta ya filamu nchini kuweza kutanua weledi ili kuwezesha sekta hiyo inakuwa zaidi na kukuza uchumi kwa taifa .
‘’SERIKALI inatoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kupanua wigo wa watalamu nakukuza weledi hivyo kukwezesha soko hili linakuwa kwa kasi zaidi’’Aliongeza GENOFEVA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni