Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Alhamisi, 3 Desemba 2015
SERIKALI :TUMESHA FANYA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA UGONJWA WA POLIO
Timothy Marko.
KATIKA Kuhakikisha malengo ya milenia ya nafikiwa katika sekta ya afya serikali imesema kuwa tayari imeshafanya utekelezaji wa maazimio ya kukomesha usambazaaji wa ugonjwa wa polio .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Dr Donarld Mmbando amesema kuwa tayari serikali kupitia wizara ya afya imewezesha utoaji wa chanjo katika kutokomeza ugonjwa huo .
‘’Tanzania imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa polio kwa kipindi cha mwaka jana ambapo Tanzania imekuwa nchi ya 35 kati yanchi 45 katika kutokomeza ugonjwa wa polio ambapo mgonjwa wa mwisho alipatikana mwaka 1996’’Alisema Katibu mkuu Donarld Mmbando .
Katibu mkuu Mmbando alisema kuwaendapo kutakuwepo na taarifa za mtoto ambaye anaulemavu unaotokana naugonjwa wa polio lazima mgonjwa huyo aripotiwe haraka katika vituo mbalimbali vya afya ilkukabiliana na ugonjwa huo.
Aidha katika hatua nyingine Dr Mmbando amewataka wananchi kufanya usafi katika maeneo yao kama agizo lilivyo tolewa na Rais Wa jamuhuri ya muungano wa TANZANIA JOHN POMBE MAGUFULI katika kuelekea maadhimisho ya siku yauhuru Desemba 9 mwaka huu kuwa ni siku ya usafi.
Alisema kuwa wizara hiyo imelipokea agizo hilo kwa mikono miwili katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ambapo agizo hili limefuatia kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu .
‘’Tukifanya usafi katika maeneo yetu hasa yanayotuzunguka tutaweza kudhibiti magonjwa ya mlipuko ,agizo la mheshimiwa Rais limekuja baada yakuwepo kwa hali ya hatari ya ugonjwa wa kipindupindu imekuwa tishio ambapo jumla ya wagonjwa 9,9609 wameweza kuripotiwa na ugonjwa huo’’Aliongeza DK mmbando .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni