Jumanne, 1 Desemba 2015

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA.

Timothy Marko. KATIKA kuhakikisha sekta ya viwanda inakuwa hapa nchini serikali kwa kushirikiana na shirikisho la viwanda pamoja nawadau wa maendeleo wakutoka nchini Japan (JICA)imetoa tunzo mbalimbali zinazo lenga kukuza sekta ya viwanda hapa nchini . Akizungumza katika ufunguzi wa utoaji wa tunzo hizo jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara uledi Mussa amesema kuwa utoaji wa tunzo hizo zinazothamini mchango wa matumizi ya dhana ya viwanda ya KAIZEN inalenga kukuza sekta hiyo yaviwanda pamoja na wataalamu wasekta hiyo ilikueweza kukuza uchumi unaotokana na sekta ya viwanda . ''SEKTA ya viwanda ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wataifa hivyo basi utoaji watunzo hizi juu yakuthamini mchango wa dhana ya Kaizen unalenga kukuza sekta yaviwanda pamoja nasekta binafsi ili kukuza uchumi wa taifa ,tunatambua kuwa sekta binfsi ndio nguzo muhimu katika kujenga uchumi ''Alisema Katibu MKuu Uledi Mussa . KAtibumkuu uledi alisema kuwa bado sekta yaviwanda pamoja nasekta binafsi zinazo mchango mkubwa lakini endapo itatumia Dhana ya KAIZEN itakuwa natija katika kujenga uchumi wa viwanda ili kuondokana na umasikini . alisema kuwa dhana hii imelenga kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mikoa ya Morogoro Dodoma pamoja na mkoa wa Dar es salaam ambapo katika kutekeleza adhima hiyo kitengo kijulikanacho kama Tanzania Kaizen Unit itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali kuptia dhana hiyo. ''mradi huu unalenga kutengeneza mipango mikakati na mbinu mbalimbali za utafiti wakisayansi katika kuboresha ubora wa bidhaa na utendaji kazi katika viwanda vyauzalishaji katika mikoa mitatu ''Alisema ULEDI MUSSA . Alisema kuwa jumla yawakufunzi wapatao42 wanatarajiwa kutoa mafunzo mbalimbali juu ya uboreshaji wasekta yaviwanda hapa nchini .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni