Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumanne, 1 Desemba 2015
KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI AWATAKA WATENDAJI WA SHIRIKA LA TRL KUJITEGEMEA KATIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU .
Timothy Marko .
SERIKALI Imelitaka shirika la reli nchini TRL kujijengea uwezo wake wenyewe katika kutengeneza vipuli vyake badala ya kuagiza vipuli kutoka nchini Afrika kusini ikiwa nimoja ya malengo yakupunguza matumizi yasiyo yalazima katika uagizwaji wa vipuli hivyo .
Akizungumza katika ziara ya kushitukiza aliyo ifanyamapema hii leo katika shirika hilo , Katibu mkuu wa wizara yauchukuzi katika shilika la reli nchini TRL Shabani Mwinjaka amesema kuwa nilazima shirika hilo lifanye tathimini ya manunuzi ya vipuli hivyo na hatimaye baada ya wiki mbili kutoa majawabu ya tathimini hiyo ya vipuli hivyo .
‘’Niwaomba mfanye thimini ya ununuzi wavipuli hivi vya reli na baada ya wiki mbili naomba nipatiwe majibu nawaagiza kufanya maboresho yakiwanda hiki ili Kujijengea uwezo ilikiweze kutengeneza vipuli ambavyo vitatumika katika ujenzi wa reli yakati ‘’Alisema Katibu mkuu Shabani Mwinjaka .
Katibu Mkuu wa wizara yauchukuzi Shabani Mwinjaka alisema kuwa nilazima shirika hilo kuunda timu maalumu juu ya utekelezwaji wa maagizo aliyo yatoa mapema hii leo katika shirika la reli nchini .
Katika hatua nyingine kaimu Mkurugenzi wa shilirika la reli nchini Elias Mshana amesema kuwa shirika hilo lipotayari katika kufanya utekelezwaji wa maagizo yaliyo tolewa na katibu mkuu shabani Mwinjaka ilkuweza kuboresha hali ya shirika hilo nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni