Ijumaa, 11 Desemba 2015

NEEC:YAMTAKA RAIS MAGUFULI KUWEKA VIPAUMBELE VYA KILIMO,MASOKO VIWANDA KUKUZA UCHUMI .

Timothy Marko. KATIKA Kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi endelevu, Baraza la Taifa linalojihusisha kutatua changa moto za uchumi pamoja na kuratibu sera za uchumi nchini, (NEEC)limemtaka Rais wa awamu ya Tano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jonh Pombe Magufuli kuweza kuanisha vipaumbele vya kiuchumi ikiwemo kuimarisha sekta ya Miundombinu katika maeneo ya vijijini yanayojihusisha na kilimo. Akizungumza katika kongamano la wadau mbalimbali wa uchumi jijini Dar es salam Muwakilishi Mkaazi wa British Council nchini Uganda ambaye pia nimtalaam wa masuala ya kiuchumi kutoka kwenye taasisi hiyo Anackel Kashuliza amesema kuwa ilkuweza kukuza sekta hiyo yakilimo na kuweza kuzalisha bidhaa zitokanazo nakilimo nilazima kuwepo namasoko yatakayowezesha bidhaa za kilimo kuweza kununuliwa ikiwemo kuimarisha sekta ya viwanda . ''Nilazima serikali ya Awamuhii ya Tano iwezekujielekeza katika maeneo ya fuatayo kilimo naviwanda napia kutojielekeza sana katika kilimo pekeyake lazima sekta kama Nishati iwekewe vipaumbele ilkuweza kuimarisha uchumi ''Alisema Anackel Kashuliza . Anackel Kashuliza alisema kuwa sekta ya Nishati vikiunganishwa na sekta ya viwanda itawezesha kuongeza uthamani wa ubora wabidhaa zinazotokana na mazao yakilimo nakuweza kuzalisha ajira kwa wingi. Alisema kuwa sekta nyinginezo ambazo zinatakiwa kuangaliwa na awamu yatano ilkukuza uchumi kwa taifa nipamoja na sekta ya Madini maji ilikuweza kukuza uzalishaji pamoja na kukuza sekta yaumwagiliaji na kuongeza uthamani wamazao yatokanayo na uvuvi nakutafuta masoko ilikuweza kukuza ajira kwa vijana . ''Nilazima sera namikakati viweze kuanishwa nakufanyiwa thathimini yakina ilkuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ilkuweza kukuza uchumi ''Aliongeza Kashuliza .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni